Sunday, 17 February 2013

 Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud walipotembelea eneo la tukio leo.Picha na Adrew Chale, Zanzibar
 Picha juu ni gari alilokua akitumia Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi leo asubuhi likiwa limegonga ukuta muda mfupi baada ya watu wasiojuliakana kumshambulia Paroko Evarist Mushi kwa risasi na kufariki
  Gari alilokuwa amepanda Padri Evarist Mushi likiwa limetapakaa damu baada ya kupigwa risasi
 Wananchi mmbalimbali zanzibar waki eneo la tukio muda mfupi baada ya gari la  Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mush kugonga ukuta baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojuliaka leo asubuhi zanzibar na kufariki
 Sehemu ya Waumini wakiwa wenye majozi muda mfupi baada ya kupata habari za kifo cha Paroko wao wa  Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mush kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana leo asubuhi  katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00
 Padri Cosmo Shayo(Kulia)akizungumza na viomgozi wa kanisa kuhusiana na tukio la Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mush kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana leo asubuhi  katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00
Picha juu na chini Sehemu ya waumini mbalimbali wakiwa nje ya viwanja vya hospitali ya mnazi mmoja leo asubuhi baada ya Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mush kushambuliwa na risasi na watu wasiojulikana leo asubuhi  katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00.Picha  Adrew Chale na Othman Maulid Othman-Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar
 Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm Nape Nnauye akizindua moja kati ya a mashina matatu aliyoyazindua leo
 MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida akizungumza
 Waziri wa Maji Prof Jummane Maghembe akiongea
 Aliyekua makamu mwenyekiti wa Bavicha Juliana Shonza akiongea
Sehemu ya umati wa wa CCM
Mfuasi mmoja wa chadema akirudisha kadi na kujiunga tena na CCM.Picha na Adamu Mzee-Idara ya itikadi na Uenezi- CCM
---
Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dar es salaam leo kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika eneo la Goba, ambapo wananchama 162 wamejiunga leo, ambapo wapo wanachama wanne kutoka Chadema walijiunga hapo hapo.

Mgeni mualikwa katika shughuli hiyo alikuwa Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi, ambaye licha ya kufungua mashina matatu ya chama, pia  aliwasaidia wakinana mama wa vikoba,shilingi milioni moja na pia kukabidhi pikipiki kwa vijana wa goba na kuahidi zingine kuwapatia karibuni.

Katika mkutano huo, Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Goba na kuwaambia sababu zilizofanya kukihama Chadema,moja ni kutotenda haki na kuwa na siasa ya kibaguzi na chuki,vurugu na uchochezi na sio kutetea watu na maendeleo.

Saumu Kisena licha ya kufanya kazi na Chadema kwa miaka 9 lakini hajalipwa haki zake hivyo ameshangazwa kuona haki inahubiriwa nje wakati ndani hakuna chembe ya usawa.
Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema na Mkurugenzi wa idara ya Habari na Uenezi -Chadema, John Mnyika
----
Kwa nyakati mbalimbali kuanzia mwezi Januari mpaka Februari 2013 pametokea matatizo ya kuharibika kwa baadhi ya mitambo na kupungua kwa uzalishaji wa maji katika vyanzo vya mto Ruvu na hivyo kusababisha matatizo ya maji kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo yanayohudumiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika Mkoa wa Pwani. 

DAWASA imeingia mkataba wa uendeshaji na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO) wa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kuendesha mitambo, kusimamia usambazaji wa maji na kufanya matengenezo na kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa. Aidha, DAWASCO wanapaswa kuzingatia mikataba ya huduma kwa wateja ambayo inaitaka kutoa taarifa kwa umma pale kunapotokea matatizo ya maji. 

Kwa kuzingatia mikataba hiyo, DAWASA na DAWASCO wanapaswa kutoa matangazo kwa umma kuhusu matatizo mapya yaliyojitokeza mwezi Januari na Februari 2013 ili kuepusha matatizo hayo kuhusishwa na hatua ya kuwasilishwa na kuondolewa bungeni kwa hoja binafsi niliyoiwasilisha tarehe 4 Februari 2013 juu ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam. 

Kwa wakazi wa Kibamba, Kwembe, Msigani, Mbezi, Saranga na Kimara ni muhimu wakatambua kwamba nimefuatilia na kujulishwa kwamba palikuwa na tatizo la kupungua kwa uzalishaji wa maji katika chanzo cha Ruvu Juu ambalo limerekebishwa tarehe 12 Februari 2013 hivyo maji yataendelea kupatikana kwa mujibu wa ratiba ya mgawo kama ilivyokuwa awali katika maeneo ambayo yalikuwa yakipata maji tangu mwaka 2012. 

Kwa wateja ambao bado watakuwa na matatizo katika maeneo yao wawasiliane na DAWASCO kupitia namba ya huduma kwa wateja 022 55 00 240 au 0779090904 au info@dawasco.com ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa. 

Kwa wananchi wa Jiji zima la Dar es Salaam ambao maeneo yao yana mabomba yanayojulikana zaidi kama mabomba ya wachina ambayo hayatoi kabisa maji kwa miaka mingi na wale ambao maeneo yao hayana kabisa miundombinu ya mabomba ya maji; hatua za haraka kwa upande wao zinapaswa kutokana na utekelezaji wa hoja binafsi niliyowasilisha bungeni. 

Hali hii inayoendelea hivi sasa ya DAWASA na DAWASCO kushindwa kufanya matengenezo ya mitambo kwa wakati na kushindwa kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa maji kwa ajili ya Jiji la Dar es Salaam kunathibitisha kwamba bunge lilipaswa kujadili hoja binafsi niliyoiwasilisha bungeni. 

Katika maelezo ya hoja pamoja na mambo mengine nilitaka Bunge ambacho ni chombo chenye wajibu wa kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi kurekebisha kasoro zilizopo katika utendaji na uwajibikaji wa Wizara ya Maji na vyombo vinavyohusika na utoaji na udhibiti wa huduma ya maji. 

Ifahamike kuwa majukumu ya utoaji wa huduma ya maji jijini Dar es salaam na baadhi ya maeneo ya Kibaha na Bagamoyo yanafanywa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ambayo ni mmiliki, mkodishaji na msimamizi wa utoaji wa huduma ya majisafi na maji taka na ina wajibu wa kupanga na kugharamia utekelezaji wa miradi ya miundombinu, kuiendeleza na kugharamia matengenezo ya dharura na makubwa. 

Mwaka 2005 DAWASA iliingia mkataba wa miaka kumi (10) wa uendeshaji na Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO). Chini ya mkataba huo majumu ya DAWASCO ni kuendesha mitambo, kusimamia usambazaji wa maji na uondoshaji wa maji taka, kuuza maji kwa wateja , kutoa ankara kwa wateja, kukusanya maduhuli, kulipia gharama za uendeshaji, kutekeleza matengenezo makubwa yanayogharamiwa na DAWASA na kutekeleza uunganishaji wa maji kwa wateja wapya kwa kutumia mfuko wa maji. 

Kisheria na kimkataba DAWASA ina wajibu wa kuisimamia DAWASCO iliyoingia nayo mkataba; hata hivyo kwa kuwa yote ni taasisi na mashirika ya umma ambayo bodi zake na watendaji wake wakuu huteuliwa na mamlaka zile zile na kuripoti kwa watu wale wale, hali ambayo ina athari kwenye utendaji na uwajibikaji. 

Wakati umefika sasa wa mkataba huo kati ya DAWASA na DAWASCO kuwekwa wazi kwa umma; kufanyiwa tathmini ya miaka zaidi ya mitano iliyopita ya utekelezaji; kufanyiwa marekebisho kwa ajili ya kipindi kilichobaki na maandalizi kuanza ya mfumo bora unaopaswa kuanza kuandaliwa baada ya kuisha kwa mkataba huo mwaka 2015. 

Izingatiwe kuwa tarehe 10 Februari 2013 niliiwasilisha kwa wananchi na kutoa wiki mbili kwa Waziri wa Maji kujitokeza kwa umma na kutoa majibu aliyokwepa kuyatoa bungeni na iwapo Waziri Prof. Jumanne Maghembe hatatoa maelezo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizarani kuwezesha hatua kuchukuliwa. 

Imetolewa tarehe 15 Februari 2013 na: 

John Mnyika (Mb)
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchini Dr Emmanuel Nchimbi akitoka chumba cha habari cha  makao makuu ya jeshi la polisi kilimani zanzibar baada ya kuongea na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari leo asubuhi kufwatia tukio la kupigwa risasi leo asubuhi Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi na kufariki dunia,Padri Evarist Mushi alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya  Nchini Dr Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari leo asubuhi katika ukumbi wa makao makuu ya jeshi la polisi kilimani zanzibar kutoka na tukio la kupigwa risasi leo asubuhi kwa Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi na kufariki dunia,Padri Evarist Mushi alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar
Sehemu ya Waandihi wa Habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar wakimsikiliza kwa Makini Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Dr Emmanuel nchimbo(hayupo picha)alipokua akitoa taarifa ya serikali kufwatia kupigwa risasi leo asubuhi kwa Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi na kufariki dunia,Padri Evarist Mushi alivamiwa na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar
 Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi 
---
Paroko wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi amefariki dunia baada ya kupigwa risasi saa 1.00 asubuhi na kufariki kabla hajafika hospitali ya Mnazi Mmoja.

Paroko huyu amepigwa risasi akishuka katika gari lake wakati akienda kuendesha ibada ya saa 3.00 leo.
Padri Evarist Mushi amepigwa risasi kichwani na kufa papohapo na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt.Theresia eneo la Mtoni Zanzibar.

Msemaji wa Jeshi Polisi Zanzibar Inspekta Mohamed Mhina amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa padre huyo ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ndipo alipofikwa na umauti huo.

Jeshi la Polisi visiwani humo kupitia kwa Msemaji wake Mkaguzi wa Polisi, Mohamed Mhina limelaani mauaji hayo na na kusisitiza kuwa Jeshi limeanza msako mkali wa kuwabaini wauaji hao.

Hili ni tukio la pili kutokea Zanzibar ambapo tukio la kwanza lilitokea kwa Padre Ambrose Mkenda kupigwa risasi na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.
Mhe. Membe akipitia Itifaki hiyo kabla ya kusainiwa huku Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akishuhudia.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiweka saini Itifaki ya Amani na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Uwekaji saini huo ulifanyika katika Hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Membe akifafanua jambo baada ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.
 Mhe. Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wake Bw. Haule. Mwingine katika picha ni Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi wa Uganda.
 Mhe. Membe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzake wa nchi za EAC wakiwa wameshikilia Itifaki hiyo mara baada ya kusainiwa
Mhe. Membe akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa