Jumuiya ya Watanzania Italia,kwa niaba ya Watanzania wanaoishi Italia, inatoa rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliofariki na waliojeruhiwa katika milipuko huko Gongo la Mboto Dar Es Salaam.
Jumuiya ya Watanzania Italia imepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa, ni imani yetu kuwa serikali yetu italitafutia ufumbuzi wa kudumu suala hili kwani ni mara ya pili sasa kutokea nchini.
Tunaamini kwamba maafa haya yamesababisha simanzi kubwa kwa nchi yetu, wakazi wa Gongo la Mboto na familia zilizokubwa na maafa haya. Jumuiya ya Watanzania Italia inawaombea wanafamilia wawe na moyo wa subira na ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa serikali na viongozi wote,mashirika , watu binafsi na viongozi wa dini kwa kuchukua hatua za haraka kuwasaidia waliokubwa na maafa,moyo huo wa kujitolea tunaomba uendelee hivyo na zaidi.
MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
Abdul Rahaman A. Alli.
Mwenyekiti.