Thursday, 21 January 2010




Siku Rais Kikwete alipojeuka Mbogo Ikulu
Jijini Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akimuliza mmoja wa wasaidizi wake Ikulu jijini Dar es Salaam juzi Bw Luambiya Fyanga Baada ya Rais Kikwete Kushindwa kutoa msaada wa Magari ya wagonjwa Aliyotaka kutoa kwa mkurugenzi wa mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Londigo kupokelewa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya ngorongoro.Picha na Fidelis Felix
---
Mambo yalikua Hivi...




''Wewe bwana unatoka wapi? alihoji Rais Kikwete na mkurugenzi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Kayange Jacob alijibu ametoka wilaya ya Ngorongoro. “Unasema unatoka Ngorongoro?" aliendelea kuhoji Rais Kikwete. "Hapa umefikaje, umekuja kufanya nini na nani kakualika? Aliendelea kuhoji huku akiwageukia wasaidizi wake akiwemo Katibu wa Rais Ikulu.


"Huyu amekuja kufanya nini hapa? Nani kamwalika", alisema Rais Kikwete ambaye sura yake ilionekana wazi kukasirika na kulazimia kuvua miwani.


Hatuwezi kukupa gari hii. Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kwa wananchi wa wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara kijiji cha Engalinaibo kipindi cha ukame ambapo nilifika Kituo cha Afya wakazi wa Engalinaibo wakaniambia hawana gari la wagonjwa na nikawaahidi nitawaletea: “Nakumbuka nilipofanya ziara wananchi wale waliniambia wanayo dispensary (Zahanati ) lakini, hawana gari la wagonjwa na sio nyinyi! Hatukupi bwana, sio lako hatukupi."


"Hatuwezi kukupa gari, watafuteni wanaopaswa kupewa gari hili, hii ni kashfa kubwa, document zote zimeandikwa kwa kijiji cha Engalinaibo iweje tuwape watu wa Ngorongoro?" alihoji.




Waombeni radhi hawa mabwana (waandishi) mliowaalika kwa ajili ya kufanya coverage hii (kuandika habari hii) kwa kuwasumbua, siwezi kutoa gari hapa waende tu, ”alisisitiza Kikwete na kuondoka eneo la tukio kwa hasira bila kukabidhi magari hayo. Baada ya tukio hilo Mwandishi Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga aliwaomba radhi waandishi wa habari kwa kuwasumbua kuhudhuria tukio hilo.



Kwa habari zaidi juu ya sakata hili zima Soma Hapa na Hapa.........>>>>>


TANGAZO
UMOJA WA WATANZANIA UINGEREZA


--

Kwa Watanzania wote madiaspora waishio Uingereza,(Ireland,Wales,England na Scotland)

Kamati ya kuandaa mchakato wa upatikanaji wa viongozi wapya wa watanzania hapa uingereza (taskforce) inawatakia watanzania wote mwaka mpya wenye neema na baraka tele.

Umoja wa watanzania hapa uingereza umekuwa ukifanyiwa tathmini kwa muda ili kuuwezesha kuwa na mwelekeo na mfumo wenye kuleta hamasa, uwazi na ufanisi zaidi katika kutumikia jamii ya watanzania hapa UK.

Kamati kwa ushirikiano na ushauri wa wadau(wanajamii) imeweza kufanya kazi kubwa ya kuleta maono na mwelekeo utakaokuwa na ufanisi zaidi katika kuwatumikia wanajamii wote hapa UK kwa kipindi hiki.

Kamati imeweza kuangalia na kurekibisha(Kupendekeza) sehemu zote muhimu zilizohitaji marekebisho ili kuleta ufanisi zaidi nazo ni kama zifuatazo:

Muundo

Uwakilishi

Katiba ya Umoja

Mwelekeo wa Umoja, na

Mfumo wa Uongozi wake.

Muundo na mwelekeo huu mpya wa umoja wa watanzania utayazingatia mambo ya muhimu ambayo ni muhimu kuyaweka wazi.

Umoja utahakikisha unaendelea kujifunza; na kuwa wazi katika utendaji wake; kuwaelimisha na kuwawezesha wanajamii wake,ili waweze kuwa sehemu ya mabadiliko na ufanisi katka jamii yetu.

Mabaadiliko ndio itakuwa changamoto yake: ili kuwa makini kukidhi mahitaji wa wadau wake.

Umoja utahakikisha unawawezesha wadau ili kuchochea umiliki na uwajibikaji wa wadau katika kuendeleza Umoja wao.

Utahakikisha unafuatilia, unatambua, kutoa nafasi na unatumia vipaji vyote vilivyo ndani ya watanzania ili kujiendeleza.

Umoja utahakikisha majukumu ya viongozi(uongozi) yanaainishwa kwa uwazi ili kuondoa miingiliano ya utendaji unaoleta mafarakano; na pia utaweka utaratibu wa kiutendaji utakaokuwa makini kulenga manufaa yawadau wake wakati wote.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa , Tafadhali watanzania waishio miji ifuatayo:

Cardiff Milton keynes
Belfast Glasgow
Northern Ireland Norwich
G. Manchester Portsmouth
Southampton Leicester
Dublin Birmingham
Luton Slough
Coventry London
Scotland Westmidlands

Tunaomba muwasiliane na kamati hii ya Umoja wa watanzania kupitia:

Email: Uniting-Communities@yahoogroups.com , au Simu zifuatazo,

Coordinator: 07766168471, Secretary: 07908010344, Members: 07799212095, or 0788841971

Tunaomba mawasiliano ili tuweze kupata watu watakaokuwa tayari kufacilitate uanzishwaji wa Umoja wa watanzania katika miji yenu.


Tafadhali anagalia kiambatanisho kwa habari zaidi. Taarifa ijayo itaambatanisha repoti ya kamati ya taskforce


Asanteni

Umoja wa Watanzania UK