Monday, 11 January 2010
Dear All

On Tuesday, January 19th, there's a special election in Massachusetts to fill Ted Kennedy's Senate seat.While the large majority of Massachusetts voters support the Democratic candidate, Attorney General Martha Coakley, special interests have poured in hundreds of thousands of dollars to mislead voters -- and the traditionally low turnout in special elections means this race could be very, very close.The stakes here are incredibly high. You know how hard we've fought and how close we've come to finally passing health reform. But also know this: To get the job done, we need Martha Coakley's vote in the Senate.No matter where you live, you can play an essential role. OFA volunteers around the country are calling key Massachusetts voters and making sure they know when and where to vote, and how important electing Martha Coakley is to the country. Each voter we reach could be the one who tips the balance.

Can you help by calling potential voters in Massachusetts?
Offering information to voters on how to participate is a great service, and it can be a lot of fun. You can take as much or as little time as you like, and no prior experience is necessary.Making these calls could be the single most important thing you can do right now to ensure the passage of health reform.But the impact of this election goes well beyond health reform -- Martha Coakley will be a vital ally to President Obama in helping our families get back to work, launching a clean-energy economy, and reining in the Wall Street abuses that still put so many Americans at risk.But it all comes down to you.

We need you to help get the word out, so please start calling today:http://my.barackobama.com/CoakleyN2N

Thank you for your help,

JeremyJeremy Bird

Deputy DirectorOrganizing for America


khitima ya mzee rashid mfaume kawawa - London
WASIFU MFUPI WA HAYATI MZEE RASHID MFAUME KAWAWA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU MSTAAFU


Mh. Rashid Mfaume Kawawa alizaliwa tarehe 27 Februari, 1926 katika kijiji cha Matepwende, Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma. Mh. Rashid Mfaume Kawawa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Fundi Mfaume Ali na Mama Zamaradi Binti Chikuse. Mzee Fundi Mfaume Ali alikuwa na mke zaidi ya mmoja. Wake wengine wawili wa Mzee Fundi walibahatika kupata watoto tisa ikiwa ni wanaume watano na wanawake wanne. Hivyo Mh. Rashid Mfaume Kawawa kwa upande wa Baba yake anao ndugu zake tisa waliozaliwa na mama wengine. Aidha kwa upande wa mama yake, Zamaradi binti Chikuse, Mh. Rashid Kawawa anaye dada yake mwingine.

4. Mzee Fundi Mfaume Ali alikuwa mwajiriwa wa Serikali kama askari wanyama pori. Mzee Fundi Mfaume Ali alipata kufanya kazi katika vituo mbalimbali katika lililokuwa Jimbo la Kusini lililojumuisha mikoa ya sasa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma. Hali hii ilisababisha Mh. Rashid Mfaume Kawawa kupata elimu yake ya msingi katika shule mbalimbali kutokana na kulazimika kufuatana na wazazi wake kila walipopata uhamisho.

5. Mh. Rashid Mfaume Kawawa alianza darasa la kwanza katika shule ya Tunduru Bomani mwaka 1935. Baada ya mwaka mmoja Mzee Fundi Mfaume Ali alihamishiwa kijiji cha Lumesule na hivyo Mh. R. M. Kawawa naye kulazimika kuhama na kujiunga na iliyojulikana kama ‘Bush School’ katika kijiji hicho. Muda mfupi baadaye Mh. Rashid Mfaume Kawawa alifuatana na wazazi wake katika uhamisho wa kwenda Kilwa Kivinje ambako alilazimika kurudia darasa la kwanza. Hata hivyo, akiwa katika shule ya Kilwa Kivinje walimu waliona kuwa alikuwa na uwezo mkubwa katika masomo na hawakusita kumrusha kwenda darasa la pili.

6. Mwaka 1940 Mh. Rashid Mfaume Kawawa alihamia shule ya bweni ya Liwale ambako alisoma hadi darasa la nne. Mwaka 1941 Mh. Rashid Mfaume Kawawa alifaulu mtihani wa darasa la nne na kuchaguliwa kuingia darasa la tano katika shule iliyoitwa ‘Dar es Salaam African Central School’ ambako alisoma darasa la tano hadi darasa la kumi.
7. Mwaka 1947 Mhe. Rashid Mfaume Kawawa alifaulu na kujiunga na shule ya Sekondari ya Tabora alikosoma darasa la kumi na moja na kumi na mbili na kuhitimu mwaka 1949. Mh. Rashid Mfaume Kawawa aliajiriwa Serikalini kwa mara ya kwanza mwaka 1949 kama Karani wa Fedha, katika kitengo cha Huduma za Maji, Dar es Salaam.

MCHANGO WA MH. RASHID MFAUME KAWAWA KATIKA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MWAFRIKA NA UHURU WA TANGANYIKA

8. Mh. Rashid Mfaume Kawawa alianza kushiriki katika harakati za kumkomboa Mwafrika tangu akiwa shuleni. Akiwa ‘Dar es Salaam African Central School’ yeye na wenzake kumi walianzisha kikundi kilichoitwa ‘United Young African Organization’ kikundi hiki kilikuwa na lengo la kuwaendeleza waafrika katika elimu, kilimo, biashara, ufugaji na michezo. Kupitia kikundi hiki yalianzishwa madarasa ya elimu ya watu wazima kuzunguka maeneo walipo wanachama wake, iwe shuleni au wakati wakiwa likizo.

9. Akiwa bado mgeni katika ajira ya Serikali Mh. Rashid Mfaume Kawawa alijiunga na Chama cha Watumishi Waafrika Serikalini mwaka 1951. Kutokana na umahiri wake katika kuendeleza shughuli na malengo ya chama hicho, Mh. Rashid Mfaume Kawawa alichaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Watumishi Waafrika Serikalini mwaka 1954. Mwaka mmoja baadaye na kwa hiari yake mwenyewe aliamua kuacha kazi Serikalini na kuingia rasmi katika shughuli za vyama vya wafanyakazi mwaka 1955. Mwaka huo Mh. Rashid Mfaume Kawawa alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tanganyika Federation of Labour). Bila shaka umahiri na kujitolea kwake katika kupinga mazingira duni ya kazi na ubaguzi ndiyo vilivyomfanya Mh. Rashid Mfaume Kawawa aonekane kuwa anafaa kushika wadhifa huo kwenye Shirikisho hilo lililojumuisha vyama vya wafanyakazi zaidi ya kumi.
10. Mnamo mwaka 1958 Mh. Rashid Mfaume Kawawa alichaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo la vyama vya wafanyakazi ambapo kupitia shirikisho hilo, alizidi kuimarisha harakati za mapambano dhidi ya mazingira duni ya wafanyakazi, hasa wafanyakazi Waafrika. Ni katika kipindi hiki ambapo ushirikiano wa Mh. Rashid Mfaume Kawawa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, wakati huo akiwa Rais wa TANU, ulipoimarika katika harakati za kuunganisha nguvu za TANU na za vyama vya wafanyakazi; kuikomboa Tanganyika kutoka utawala wa kikoloni.

11. Mwaka 1957, TANU ilimchagua Mh. Rashid Mfaume Kawawa kuwa mmoja wa Wawakilishi wake katika Baraza la kutunga sheria katika Serikali ya Mkoloni. Akiwa mjumbe katika baraza hili Mh. Kawawa alipata nafasi ya kuibana Serikali katika mambo kadhaa ikiwemo kuitaka Serikali:-
· Kuvisikiliza na kuvitambua vyama vya wafanyakazi;
· Kutunga sheria za usalama kazini; na,
· Kuhakikisha kuwapo haki ya elimu kwa wafanyakazi
MCHANGO WA MH. KAWAWA KATIKA KULITUMIKIA TAIFA


12. Pamoja na kufanikiwa kuwaunganisha Watanzania kudai na hatimaye kupata uhuru, mchango wa Mh. Kawawa katika kuijenga Tanzania huru uliendelea kuwa mkubwa kama ifuatavyo:

· Mwaka 1960 Mh. Kawawa aliteuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa na Nyumba kwenye Serikali ya Madaraka iliyoundwa na Rais wa TANU.
· Mwaka 1961 Mh. Rashid Mfaume Kawawa aliteuliwa kuwa Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo moja ya majukumu yake ilikuwa ni kusimamia mpango wa kugawa madaraka kwa waafrika (Africanization).
· Mwaka 1962 mwezi Januari, Mh. Kawawa alichukua wadhifa wa Waziri Mkuu kufuatia Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kujiuzulu wadhifa huo ili aende kuimarisha TANU.
· Mwezi Desemba, 1962 Mh. Rashid Mfaume Kawawa aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais baada ya nchi kuwa Jamhuri chini ya Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
· Baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwaka 1964, Mh. Rashid Mfaume Kawawa aliteuliwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais na pia akIwa na dhamana ya Waziri wa Ulinzi. Alitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kipindi hicho na kujenga misingi imara ya jeshi hilo. Aidha alianzisha pia Jeshi la Kujenga Taifa.


· Mwaka 1972 Mh. Kawawa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wadhifa alioendelea nao hadi mwaka 1977 alipoteuliwa tena kuwa Waziri wa Ulinzi.
· Pamoja na majukumu haya Mh. Kawawa aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea na baadaye Liwale kati ya mwaka 1965 – 1985.

MCHANGO WA MH. RASHID MFAUME KAWAWA KATIKA KUKITUMIKIA CHAMA CHA TANU NA BAADAYE CCM


13. Mh. Rashid Mfaume Kawawa alijiunga na TANU tangu akiwa mtumishi wa Serikali, licha ya kuwa jambo hili halikuruhusiwa na Serikali ya kikoloni. Mh. Kawawa alichaguliwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU mwaka 1958. Mh. Kawawa alishika nyadhifa mbalimbali katika chama cha TANU hadi CCM. Nyadhifa hizo ni pamoja na:-

· Makamu wa Rais wa TANU;
· Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM;
· Makamu Mwenyekiti wa CCM;
· Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa CCM;
· Kamanda Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Taifa toka 2003 hadi umauti ulipomfika;
· Hadi kifo chake Mh. Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Mjumbe wa Kudumu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

14. Mh. Rashid Mfaume Kawawa ndiye aliyeanzisha rasmi Umoja wa Vijana wa TANU mwaka 1958 akiwa Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja huo.

15. Katika utumishi wake ndani ya TANU na baadaye CCM, Mh. Rashid Mfaume Kawawa alishiriki katika kufanya maamuzi ya mambo mbalimbali makubwa na kusimamia utekelezaji wake kwa ujasiri mkubwa ambao unajionyesha katika maeneo muhimu ya historia ya Taifa letu.

16. Mhe. Rashid Mfaume Kawawa atakumbukwa na ametufundisha mengi yakiwemo:

· Uzalendo wa hali ya juu, uaminifu, utiifu katika kulitumikia Taifa kwa dhati.
· Kuwa na mioyo ya subira na ustahimilivu.
· Kuacha mioyo ya tamaa iliyopita kiasi na kuweka mbele maslahi ya Taifa.
· Nidhamu ya utekelezaji wa mambo mbalimbali.
· Uchapakazi hodari, ubunifu na kujituma kwake uliojionyesha alivyochochea kuanzishwa kwa Umoja wa Vijana wa TANU na Jeshi la Kujenga Taifa.17. Mhe. Rashid Mfaume Kawawa alistaafu rasmi shughuli za uongozi wa Serikali na katika Chama cha Mapinduzi mwaka 1993 alipoacha umakamu mwenyekiti wa CCM. Pamoja na kuwa na umri mkubwa Mh. Kawawa hata baada ya kustaafu aliendelea kuwa mfano wa kuigwa katika shughuli za kujiletea maendeleo kwenye kilimo, ufugaji, uvuvi na ushirika. Wananchi kutokea sehemu mbalimbali nchini walifika nyumbani kwa Mh. Kawawa kujionea jinsi shughuli hizo zinavyoweza kuendeshwa kitaalam na kutoa tija kwa wahusika.
18. Katika uhai wake Hayati Mh. Rashid Mfaume Kawawa alioa wake watatu na kujaliwa kupata watoto kumi na tano. Wawili kati ya wake zake Mama Sofia Kawawa na Mama Asia Kawawa walishatangulia mbele za haki hivyo Mh. Kawawa ameacha mjane Bi Asina, watoto 15 na wajukuu 36 na vitukuu 4.
19. Mh. Kawawa atakumbukwa kama mmoja wa Waasisi Mashuhuri wa Taifa letu ambako mchango wao ndio umetuwezesha kufikia maendeleo tunayoshuhudia sasa.


MUNGU AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA, AMINA.