Thursday, 12 June 2008

ajali ya ndege Tanzania

Footballer Samuel Etoo in Tanzania


AJALI YA NDEGE TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
--------
Rais Jakaya Kikwete leo Juni 11, ameongoza waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu waliofariki dunia katika ajali ya helikopta ya jeshi iliyotokea Jumatatu wiki hii mkoani Arusha.
Miili ambayo iliagwa rasmi ni ya rubani wa helikopita hiyo Kanali Wakete, msaidizi wa rubani Meja Sinda, rubani msaidizi na fundi ndege Luteni Kirunga pamoja na Bibi Irene Nkamba Jitenga, mke wa Brigadia Jenerali Jitenga ambaye ndiye mkuu wa vikosi vya JWTZ kanda ya kaskazini.
Rais Kikwete alikwenda kuaga miili hiyo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema asubuhi akitokea mjini London Uingereza ambako alihudhuria kikao cha wakuu wa nchi 10 za Jumuiya ya Madola kilichomalizika jana.

Rais Kikwete alipokelewa uwanjani hapo na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamu Rais Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia aliungana na Rais katika kuwaaga wahanga hao huku Ukonga Air Wing jijini Dar es salaam Miongoni mwa waliohudhuria kuaga miili hiyo ni pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamnyange,Inspekta Jenerali wa polisi Said Mwema na maafisa mbali mbali wa jeshi.Miili hiyo ilitarajiwa kusafirishwa kwenda Mwanza,Musoma na Iringa kwa ajili ya mazishi.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar Es Salaam
Tanzania
11 Juni 2008






Uganda President Yoweri Museveni speaking to the Promota Africa Magazine

The celebration of the ethiopia Millennium at the ethiopia embassy in London




Ayoub mzee with Dr Knox of theInstitute of defence and strategic Stadies







Photos: Ayoub Mzee

Albino's Plight in Tanzania


http://www.nytimes.com/2008/06/08/world/africa/08albino.html?bl&ex=1213070400&en=751c11f3322c497f&ei=5087%0A