Wednesday, 4 September 2013

Government leaders make case for limited military action
Secretary of State John Kerry speaks with Chairman of the Joint Chiefs of Staff Martin E. Dempsey during a Senate Foreign Relations Committee hearing at the Hart Senate Office building in Washington D.C., Sept. 3, 2013. President Barack H. Obama is seeking congressional approval for a limited military strike in Syria in response to their government's alleged use of chemical weapons. (Department of Defense Photo by Mass Communication Specialist 1st Class Daniel Hinton)


Read more: http://www.dvidshub.net/image/1009323/government-leaders-make-case-limited-military-action#.UiZ9YDamivg#ixzz2dsYTqYfb


Please find enclosed the S3  of the Senate Foreign Relations Hearing Opening Statement by US Secretary of State John Kerry at the SFRC Hearing to examine the authorization of use of force in Syria.



Press Note:
Tuesday, Sep. 03, 2013
2:30 PM -  Foreign Relations
Hearings to examine the authorization of use of force in Syria. 
SH-216        

Hearing The Authorization of Use of Force in Syria
U.S. Senate Committee on Foreign Relations
Presiding: Senator Menendez
Date: Tuesday, September 03, 2013
Time:02:30 PM
Location: Senate Hart 216

The Honorable John F. Kerry
Secretary of State
U.S. Department of State
Washington, DC




The following files are available for download.


=================================
03-sfrcKerry-s3.mov (530.90MB)



=================================
03-sfrcKerry-s3.mp3 (18.90MB)



=================================
03-sfrcKerry-s3.wmv (686.52MB)

--

DAILY NON-STOP FLIGHTS FROM DAR TO ARUSHA & MTWARA
On our new 19-seater Beechcraft

                       Waziri Membe akutana na Uongozi wa APRM Tanzania

image

Mhe Waziri leo amekutana na uongozi wa APRM Tanzania. Ujumbe huo chini ya Mwenyekiti Prof. Hassa Mlawa, umetumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Waziri Membe kwa ushirikiano alioutoa yeye kama Focal Point wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara kwa ujumla, ikiwemo kulipwa kwa deni la muda mrefu la mchango wa Tanzania katika Sekretariati ya APRM na kuliondolea taifa aibu. 

Aidha, Ujumbe huo ulitumia fursa hiyo kumueleza Mhe. Waziri juu ya hatua zinazofuata katika utekelezaji wa yatokanayo na Ripoti ya Tathmini ya Tanzania.

Mhe. Membe alipongeza Uongozi wa APRM kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa uadilifu mkubwa na kuiletea Tanzania heshima. Ametumia fursa hiyo kuwahakikishia ushirikiano wa Wizara yake katika kuratibu utekelezaji wa yatokanayo na Ripoti hiyo. Amewataka APRM kusambaza taarifa hiyo kwa wananchi na wadau wote kwa kuwa taarifa hiyo ni ya umma.



Kufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.Zuberi Mgeni Zuberi
alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa 
Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 
kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni. Shughuli wanazo fanya ni Uvuvi na Ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya 
chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua 
Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwahiyo walikuwa wa kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea  na Masomo ya Sekondari ndipo hapo 
Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika Mwaka 2011 Juni. 
Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo. Chakusikitisha nikuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa Tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6000 za Kimarikani sawa na Shs.9,600,000/= za Tanzania.Zikipatikana anaweza kusafirishwa na Msaidizi wake mmoja. Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia Nambari zifuatazo:- 0777 980492 au  
0714 980492 Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui  na Mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662. Msaada wa ki Fedha unaweza kutumwa kwenye Akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa Fedha za Kigeni 
 Bank ya Exim Tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.
Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.
   SHUKRAN
Yunus Chui. 

Tuesday, 3 September 2013

KWAHERI CHADEMA, KARIBU CCM DADAKE MBOWE:

DADA YAKE FREEMAN MBOWE ARUDISHA KADI YA CHADEMA,AJIUNGA CCM NA KUKABIDHIWA KADI YA UANACHAMA


Picture: Grace Mbowe
DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za 
kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
Picture: Grace Mbowe, Hassan Mtenga
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea.

 Source HabariLeo

Monday, 2 September 2013

MAGAZETI YA BONGO LEO...2/9/2013




.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
All Set for 2nd EAC University Students' Debate

East African Community Secretariat, Arusha, 30 August 2013: The 2nd EAC University Students’ Debate on Regional Integration is slated for 2 – 3 September 2013 next week at the at Belmont hotel in Dar es salaam, Tanzania.
The Debate whose theme is: “Understanding the Opportunities and Challenges arising from the EAC Integration for Youth in East Africa” aims at promoting continuous dialogue among the youth and to interest them in advocating for regional integration initiatives

The debate is expected to  bring together representatives from academia, private sector, civil society, media and technocrats from the East African region who will listen to the debate and make their comments on the strength of the deliberations and make recommendations on the way forward for the debate

The Debate involves six participants from each EAC Partner State, drawn from national universities, both public and private and other institutions of higher learning. The participants will choose to be either on the opposition or proposition side.

The EAC University Students’ Debate will be moderated by three judges with expertise on the specific area of discussion  on the overall area of EAC and political integration.

The two-day function will be capped with a gala dinner, at which the best debaters will be presented with awards and also appointed as EAC Youth Ambassadors 2013/2014 with an obligation to spear head peer to peer learning in their respective universities in collaboration with the EAC Secretariat and EAC Ministries in the Partner States.

KIFO CHA MBARAKA KILITUMIWA KISIASA?


Katika miaka ya 70 mwishoni kulikuweko na mgogoro mkubwa kati ya Tanzania na Kenya, mgogoro ambao ulifikia hata kufunga mipaka kati ya nchi hizi mbili. Malumbano makali ya kisiasa yaliendelea katika vyombo vya habari vya nchi hizi mbili, na ilifikia kuwa  kila upande ulilaani siasa za nchi nyingine, kati ya malumbano ninayoyakumbuka ambayo yaliyokuwa yakiendelea katika radio ni pale Tanzania ilipoiambia Kenya kuwa ni nchi ya Manyang'au yenye utaratibu wa ‘Man eat man society’, nao Kenya wakajibu Tanzania ni nchi ya ‘Man eat nothing society’. Vibonzo vya magazeti ya Kenya vilijaa picha za kejeli kwa nchi ya Tanzania, na kibonzo kimoja kikionyesha kiongozi wa China Mao Tse Tung akiwa amempakata Mwalimu Nyerere, wakati Mzee Kenyatta akionekana akitoka mbio kali, viliiudhi sana serikali ya Tanzania.
Nia ya madhumuni ya habari ninayoandika hapa ni Je, siasa ilihusika katika kutoa maelezo ya kifo cha Mbaraka Mwinyshehe?
Katika miaka yote kutokana na maelezo yaliyotolewa na vyombo vya habari vya Tanzania, ilionekana kuwa kama Mbaraka angepewa matibabu aliyostahili angeweza kupona, na kuwa  kilichosababisha kifo chake ni kunyimwa damu kwa kuwa Mbaraka alikosa fedha za kulipia damu katika hospitali aliyokuwemo. Katika chambua chambua zangu nimepata nakala ya maelezo aliyotoa mwanamuziki mmoja Mtanzania aliyeshuhudia ajali na kushiriki hata kuwaita wanamuziki wa Mbaraka kwenda hospitali aliyofia marehemu yananipa picha tofauti na niliyokuwa nayo miaka yote.
Zebedee Japhet Kinoka au maarufu kama Super Zex ni mwanamuziki wa siku nyingi sana ambae pamoja na bendi nyingine aliwahi kupigia Amboni Jazz, Salna 5 Brothers za Tanga na Villa Negro iliyokuwa na maskani Mombasa japo iliongozwa na wanamuziki kutoka  Tanga. 
Kwa maelezo yake mwenyewe mwazoni mwaka 1979 aliamua kuvuka mpaka na kwenda Mombasa katika kutafuta maisha kimuziki. Siku ya tarehe 12 Januari 1979 alikuwa anatoka maeneo ya Kisauni kumtembelea Mtanzania mwenzake aliyekuwa na hoteli huko,  ambaye pia walitoka kijiji kimoja Malamba  huko Tanga. Anasema alipofika karibu na  Kongoya Church aliona gari aina ya Peugot 404 nyeupe ikitoka upande wa Bush Bar na kwa spidi kali ikaenda na kuligonga roli moja lililokuwa  likitokea  upande mwingine. Ilikuwa mchana kiasi kama saa 7 hivi. Watu wakakimbilia kungalia ajali akiwemo yeye. Na mara moja akamtambua Mbaraka na kuwambia watu kuwa huyo ni mwanamuziki Mtanzania anaitwa Mbaraka Mwinyshehe. Katika gari lile kulikuweko watu watatu Mbaraka alikuwa amekaa mbele pamoja na dereva. Dereva na pasenja aliyekuwa nyuma walikufa palepale, ikalazimika kuanza kukata mabati ili kumuondoa Mbaraka aliyekuwa amebanwa miguu katika gari lile lililoharibika, yeye alikuwa bado hai. Wakati kazi hiyo inaendelea Zebedee alikimbilia Kengeleni Bar ambapo Jamhuri Jazz Band ( Bendi ya Watanzania) ilkuwa ikipiga muziki nakuwambia kuwa mwenzao kaumia sana, nao wakatoka mbio, wakiwemo akina Harrisson Siwale. Mbaraka aliweza kutolewa kwenye gari na kupelekwa kwenye hospitali ya Makadara. Zebedee pia akatumwa kuwafuata wanamuziki wa bendi ya Super Volcano ambao wakati huo walikuwa wakipiga Zambia Bar, wanamuziki walipofika hospitali wakaambia watoe damu na wakaanza kukwepa kutoa damu kwa visingizio mbalimbali. Muda si mrefu Mbaraka Mwinyshehe akafariki. Mbaraka alifarika 12 Januari 1979 akiwa na umri mdogo wa miaka 34 tu. Hakuna maelezo popote ya huyu shahidi kuwa kukosekana kwa pesa ndio kilikuwa sababu ya kifo cha Mbaraka

Sunday, 1 September 2013

RWANDA YAFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA TANZANIA.......


Dk. Benjamin (Ben) Rugangazi, Balozi wa Rwanda nchini Tanzania na Shelisheli amezungumza na gazeti hili la Raia Mwema kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo nchi hizi mbili. Yafuatayo ni mahojiano kamili baina mwandishi wa gazeti hili, Ezekiel Kamwaga na mwanadiplomasia huyo ambaye kitaaluma ni daktari wa mifugo.
Raia Mwema: Mheshimiwa Balozi, matamshi ya viongozi wa juu wa nchi hizi mbili katika siku za karibuni yanaonyesha kwamba hali ya uhusiano baina ya Rwanda na Tanzania si nzuri kwa wakati huu. Je, wewe unalionaje hili?
Dk. Rugangazi: Nashukuru kwa swali lako. Kusema ukweli, hali ya uhusiano baina ya nchi zetu ni nzuri na ndiyo maana leo tunazungumza hapa bila matatizo yoyote.
Hata hivyo, niseme kwamba baadhi ya vyombo vya habari vinalikuza suala hili. Nitoe mfano wa makala moja iliyoandikwa na mwandishi aliyejiita Abdul Majid kwenye gazeti lenu ambayo ilizungumza mambo mengi yasiyo mazuri.
Makala ile kwa kweli haikutenda haki kwa Rwanda, kwa Rais Paul Kagame na kwa uhusiano mwema wa Tanzania na nchi yangu. Mambo mengi yalikuwa ya upotoshaji.
Vyombo vya habari vina wajibu wa kuchochea uhusiano mwema na sisi kama taifa ni wahanga wa uhasama uliochochewa na vyombo vya habari. Hata mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994, yalichochewa sana na vyombo vya habari.
Raia Mwema: Makala unayoizungumzia iligusia suala la madai ya muda mrefu kuwa mauaji ya aliyekuwa Rais wa Rwanda, Juvenal Habyarimana, yalifanywa na kundi la RPF ambalo sasa ndilo linaloongoza serikali ya nchi hiyo. Unazungumziaje kuhusu madai haya?
Dk. Rugangazi: Huo ndiyo upotoshaji ninaouzungumzia. Kuna tume ilifanya uchunguzi na ambayo taarifa yake ilitolewa na ipo hadharani kwamba bomu lililolipua ndege ya marehemu Habyarimana lilitokea katika maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kigali.
Kwa wakati huo, uwanja huo ulikuwa ukishikiliwa na majeshi ya serikali pamoja na yale ya Ufaransa. RPF haikuwepo kwenye eneo hilo na ndiyo maana ripoti ikasema RPF haihusiki.
Huo ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi kabisa.
Raia Mwema: Chanzo cha tofauti ya sasa baina ya nchi yako na Tanzania kinaelezwa kuwa ni hatua ya Rais Jakaya Kikwete kushauri mzungumze na kundi la waasi la FDLR. Kuna ugumu gani kwenu kuzungumza na kundi hilo?
Dk. Rugangazi: Kwanza niseme mapema kwamba suala la sisi kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR halipo kwenye ajenda yetu. FDLR ni kundi la waasi ambalo dhamira yake ni kufanya mauaji mengine ya kimbari dhidi ya wananchi wa Rwanda.
Tofauti iliyopo baina ya serikali na FDLR si ya kisiasa wala si ya ugomvi wa kawaida. Ni tofauti kwamba kuna watu hawataki wenzao waishi hapa duniani na wengine wanataka kuishi na kuendeleza taifa lao.
Tatizo la sisi na FDLR nalilinganisha na tatizo la Wayahudi na Manazi wa Ujerumani. Huwezi leo ukasema Wayahudi wakae na kupatana na manazi maana hawana matatizo ya kuyajadili wakayamaliza.
Wanazi wanataka Wayahudi wafutike kwenye uso wa dunia. Hiyo ndiyo sera waliyokuzwa nayo. FDLR ni wauaji na huo ndiyo mtazamo wetu.
Hata hivyo, tumesema kwamba wale wapiganaji wa FDLR ambao wako tayari kukiri makosa yao na kutubu, tunaweza kuwasamehe na kujenga upya nchi yetu. Tumefanya hivyo tayari na ndiyo maana waasi zaidi ya 51,000 wamerejea Rwanda wakitokea katika kundi la FDLR katika kipindi cha kati ya mwaka 1996 hadi sasa.
Baadhi yao wameingizwa katika Jeshi la Rwanda na hivi ninavyozungumza na wewe, Mkuu wa Magereza nchini Rwanda alikuwa askari wa zamani wa FDLR.
Wale ambao hatuwezi kuzungumza nao ni wale ambao wana mashitaka ya kujibu kutokana na makosa waliyoyafanya kwenye mauaji ya mwaka 1994.
Wale ambao bado wanataka kufanya mauaji ya kimbari na hawataki kukiri makosa yao hatuwezi kuzungumza nao.
Raia Mwema: Kama mmeweza kuchukua watu 51,000 na wengine mkawapa madaraka makubwa, mnashindwaje kuzungumza na hawa wengine?
Dk. Rugangazi: Kuna watu waliua na wameshitakiwa kwa makosa waliyoyafanya na hawa ambao wana mashitaka ya kujibu ni lazima sheria ichukue mkondo wake.
Kuna watu ambao hadi Umoja wa Mataifa (UN) umetangaza kwamba wanatafutwa na kama unavyofahamu, serikali ya Marekani imetoa hadi zawadi kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwao.
Kama wanadhani wanaonewa, wajitokeze na waende kujibu mashitaka yao kwenye Mahakama ya Kimataifa kama wenzao waliopelekwa ICTR ya Arusha. Kama wakishitakiwa huko na wakakutwa hawana hatia na wakaonyesha kuwa hawana nia wala mwelekeo wa kutaka kuangamiza Wanyarwanda hapo tunaweza kuwa na mawazo mengine.
Lakini katika hali ya sasa, hakuna cha kuzungumza nao.
Genocide is not an ordinary crime. It is not fighting to defeat. It is killing to decimate (Mauaji ya kimbari si uhalifu wa kawaida. Si kupigana kwa lengo la kushinda vita. Ni mauaji yenye lengo la kuhilikisha (kuwafuta kabisa kwenye uso wa dunia) wapinzani wako.
Hii ndiyo sababu tunasema waliohusika na mauaji ya kimbari ni watu ambao kwanza wanatakiwa kukumbana na mkono wa sheria kabla ya mambo mengine.
Raia Mwema: Kuna taarifa kwamba serikali yenu haikufurahishwa na hatua ya Tanzania kupeleka askari wake kwenye kikosi cha kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Kuna ukweli kwenye hili?
Dk. Rugangazi: Si kweli. Rwanda inaunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU) kwenye kuleta amani nchini DRC. Hivyo hatuna tatizo na uwepo wa Tanzania.
Raia Mwema: Nina taarifa kwamba serikali yenu ilituma ujumbe kwa serikali ya Tanzania kuomba isitishe mpango wake wa kupeleka askari Rwanda. Vyanzo vyangu vinaniambia kwamba serikali ya Tanzania ilikataa. Unazungumziaje suala hili?
Dk. Rugangazi: Mimi ndiyo nasikia kutoka kwako hizo taarifa. Kama mimi balozi ndiyo nasikia kwako suala hili kwa mara ya kwanza, maana yake ni kwamba suala lenyewe halipo.
Maana kama ujumbe umetumwa na serikali ya Rwanda kuja Tanzania, mimi nitakuwa mtu wa kwanza kujua. Huo ndiyo ukweli. Serikali ya Rwanda haikutuma watu kuja Tanzania.
Raia Mwema: Kuna madai kwamba hamkutaka Tanzania iende huko kwa sababu mna uhusiano wa karibu na kundi la M23 ambalo ndilo hasa linaloleta matatizo Mashariki mwa Congo. Je, ni kweli kwamba mnalisaidia kundi hilo?
Dk. Rugangazi: Huo ni uzushi mwingine wa NGO’s zilizoko DRC. Taarifa hizi zinaandikwa sana kwenye vyombo vya habari vya Ulaya na Marekani. Jibu langu kwa swali lako ni moja tu; Nenda mwenyewe Mashariki mwa DRC na ukahakikishe. Hatutoi msaada wowote kwa M23.
Kuna mambo yao wenyewe na serikali ya DRC ambayo yanatakiwa yamalizwe lakini Rwanda haitoi msaada wowote. Uhusiano pekee uliopo ni kwamba lugha kubwa inayozungumzwa katika maeneo hayo ni Kinyarwanda.
Raia Mwema: Rais Kagame analaumiwa kwamba siku hizi ni dikteta na hafuati misingi ya utawala bora. Una maoni gani kuhusu hilo.
Dk. Rugangazi: Nani anayemlaumu?
Raia Mwema: Hata Jenerali Kayumba Nyamwasa anadai hivyo.
Dk. Rugangazi: Namfahamu Nyamwasa kwamba ni mtu ambaye alishindwa kutimiza majukumu yake. Ameanza kulalamika mara tu baada ya kuvuliwa nyadhifa zake. Kama angekuwa mkweli, angeyasema anayoyasema wakati akiwa na vyeo vyake vyote jeshini.
Niseme tu kwa ufupi kwamba rekodi ya Rais Kagame iko wazi. Rwanda imetoka katika kipindi kigumu sana lakini imepata maendeleo ya haraka ambayo yanapigiwa mfano.
Hata hivyo sisemi kwamba eti Rwanda inajihisi inaonewa wivu kutokana na maendeleo iliyoyapata kama ambavyo ile makala ya kwenye gazeti lenu ilivyodai.
Rwanda bado ni nchi masikini na Rais Kagame halali usingizi kwa ajili ya hilo. Ukweli wa wazi kabisa ni kwamba Rwanda na Tanzania bado ni nchi masikini na zinahitaji sana kushirikiana ili kujiongezea maendeleo.
Raia Mwema: Sawa Nyamwasa hakutimiza majukumu, lakini madai kama hayo yamewahi kutolewa pia na wanasiasa wengine wakubwa tu wa Rwanda. Watu kama Seth Sendashonga miaka ya nyuma na Theogene Rudasingwa. Wote hawa pia walikuwa na uchungu wa kunyimwa madaraka?
Dk. Rugangazi: Ok. Kwanza niseme kwamba siwezi kukaa hapa na kukupa majibu ya watu wote ambao wamewahi kupingana na Rais Kagame miaka ya karibuni au zamani.
Ninachokifahamu ni kwamba Rais Kagame ni mchapakazi na ana nia ya kuibadili Rwanda na Wanyarwanda ili wawe bora kuliko alivyowakuta. Kwenye hili, yuko tayari kuhatarisha mahusiano yake binafsi na watu kwa ajili ya faida ya taifa lake.
Raia Mwema: Wewe ni balozi na unazungumza na Rais Kagame wakati wowote na pia unazungumza na Rais Kikwete pale unapohitajika. Kuna madai kwamba viongozi hawa wawili hawana mahusiano mazuri. Unazungumziaje hili?
Dk. Rugangazi: Nisingependa kuzungumzia mahusiano binafsi ya viongozi wangu. Nawaheshimu sana na si kazi yangu kuhakikisha viongozi wana mahusiano mazuri au mabaya.
Kilicho cha muhimu kuliko vyote ni wananchi zaidi ya milioni 150 walioko ndani ya nchi hizi mbili. Kama wananchi hawa wakiwa na uhusiano mzuri, sote tutafaidika.
Nadhani hilo ndilo ambalo nimetumwa kulifanya hapa. Kuhakikisha Rwanda na Tanzania zinakuwa na uhusiano mzuri kiuchumi, kisiasa, kijamii na katika nyanja zote za muhimu.
Raia Mwema: Unakumbuka nini kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994? Kuna ndugu, jamaa au marafiki uliopoteza kwenye mauaji hayo?
Dk. Rugangazi: Ndiyo. Kimsingi, sidhani kama kuna Mnyarwanda ambaye hakupoteza ndugu, jamaa au marafiki wakati wa mauaji hayo. Ninachokumbuka zaidi ni kuona miili ya watu waliouawa kikatili ikiwa imezagaa barabarani.
Kuna wengine waliouawa walikuwa watoto wanaotambaa. Mtu anachukua panga na kumuua mtoto ambaye anatambaa kumfuata kuomba msaada.
Sasa unajiuliza huyu mtoto mchanga anayetambaa ana makosa gani ya kuuawa kikatili namna hii? Siku moja nilikuja kwenye shughuli za utoaji wa misaada ya kijamii hadi mpakani mwa Tanzania na Rwanda upande wa Kagera.
Kwenye mto Kagera nikaona maiti zinapita. Kuna maiti moja ikawa inapita kwenye mkondo wa maji unaozunguka. Maiti ikawa inazungushwa tu bila ya kwenda popote. Kwa kweli nililia sana siku ile.
Na niseme ukweli, tangu wakati huo, imani yangu kwa Mungu iliingia kwenye wakati mgumu sana. Nilijiuliza, hivi kweli kama yupo anaruhusu vipi watu wake wateseke namna hii? Maiti ile ina makosa gani. Watoto wale wachanga wana makosa gani?
Na unajua walikuwa wanajuaje kama huyu ni Mhutu au Mtutsi? Vitambulisho. Vitambulisho vilivyokuwepo vilikuwa vinaandikwa kama mtu ni wa kabila gani. Hivyo wauaji walikuwa wanasimamisha magari na kukagua vitambulisho. Wale waliokuwa wameandikwa Wahutu walikuwa wakiuawa hapohapo.

Chanzo :- Raia Mwema

- See more at: http://www.raiamwema.co.tz/rwanda-yafunguka-kuhusu-uhusiano-wake-na-tanzania#sthash.XZAgdlum.dpu

BREAKING NEWS: NDEGE ZAGONGANA ZANZIBAR AIRPORT.

Ndege ya Oman air na Ethipian airlines leo jioni zimegongana katika kiwanja cha ndege cha Zanzibar wakati zikijitaarisha kuruka, ila ajali hii haikuwa kubwa, wakati hayo yakiendelea abiria wa Ehiopian airline wameshushwa na kuweka sehemu ya mapumziko.
Nawatakia kila la kheri wasafiri wote na inshaalah Mwenyezi 
Mungu atawapa wepesi wa katika safari zao.
Ndege ya kulia ni ya Ethiopian airlines ambayo ndiyo imeivaa Oman air hadi bawa kutoka.

IGP ASAFISHA VIGOGO UWANJA WA NDEGE.

Dar es Salaam. Siku chache baada ya kuibuliwa kwa kashfa ya kupitishwa kiholela kwa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jeshi la Polisi limemwondoa Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Kamishna Msaidizi (ACP), Deusdedit Kato pamoja na Mkuu wake wa Upelelezi, David Mwafwimbo.
Mbali ya maofisa hao, pia jeshi hilo limemwondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa, naye ikiwa ni miezi michache baada ya kutokea kwa ghasia wakati baadhi ya wakazi wa huko walipokuwa wakipinga mpango wa Serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Nafasi ya Kamanda Sinzumwa imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Zelothe Stephen kutoka Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema amemteua, ACP Selemani Hamisi kuchukua nafasi ya Kato ambaye anahamishiwa makao makuu ya jeshi hilo. Kabla ya uteuzi huo, Kamanda Hamisi alikuwa Makao Makuu Idara ya Upelelezi.
IGP Mwema pia amemteua Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad kuchukua nafasi ya Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).
Taarifa hiyo ya Polisi ilisema uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo yake. Hata hivyo, katika siku za karibuni, kumekuwa na malalamiko mengi kuwa vyombo vya usalama katika uwanja huo vimeshindwa kudhibiti biashara hiyo na matokeo yake Tanzania imechafuka katika medani ya kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana wake kukamatwa sehemu mbalimbali duniani.
Matukio ya karibuni yanahusisha kukamatwa kwa wasanii Agnes Masongange na Melisa Edward waliokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Johannesburg, Afrika Kusini.
Kutokana na kashfa hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliamua kulivalia njuga suala hilo na kuchukua hatua kadhaa na pia alifichua jinsi wasichana hao walivyosaidiwa kupitisha dawa hizo na mtandao uliohusisha polisi, maofisa usalama wa taifa na baadhi ya wafanyakazi wa JNIA.
RPC Mtwara
Sinzumwa anaondoka Mtwara baada ya ghasia kubwa zilizozuka Mei mwaka huu wakati baadhi ya wakazi wa Mtwara walipokuwa wakipinga gesi kutoka Msimbati kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.
Katika ghasia hizo, ambazo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), liliingilia kati, polisi walishutumiwa na wakazi wa huko kwa kutumia nguvu kubwa na kuwasababishia madhara.
Mwananchi



 President Jakaya Mrisho Kikwete walks with  Ms Kristalina Georgieva, the  European Commissioner for International Cooperation and Humanitarian Aid, shortly before the start of the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.
 President Jakaya Mrisho Kikwete walks with Dr Jeffrey Sachs, Director of Earth Institute at the Columbia University, as they head to the meeting hall to  attend the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete with Mr Manuel Jose Barroso, President of the European Commission, at the start of the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete attends the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013. Left are members of his delegation, Professor Rwekaza Mukandala, Vice Chancellor of the University of Dar es salaam and Profesor Joseph Semboja, Principal Uongozi Institute.
 President Jakaya Mrisho Kikwete attends the High-level Retreat on "New Ideas for a Fair Globalization in Alpabch, Austria August 30, 2013. Right is the host and Co-Chairman of the Retreat, Mr Manuel Jose Barroso, President of the European Commission, followed by Ms Valerie Amos, UN Under-Secretary-General of for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator
State House Photos

Witness: A Boy's Mining Accident – Richard’s Story


Photo © 2013 Justin Purefoy for Human Rights Watch 

Richard, 11 years old at the time, was down in the gold mine pit when he heard his friends yelling for him to get out. Before he could react, he saw the landslide – caused by a collapsed wall – rushing toward him. The earth rammed into him and buried him up to his chest. Other miners hurried to dig Richard out, and he was taken to the nearest hospital where they diagnosed him with internal injuries. Even today, a year and a half later, the pain in his mid-section sometimes makes it hard for him to walk.
Richard’s story is familiar to people of rural southern Tanzania, where noisy, bustling towns seem to spring up in the middle of a sea of dried grass around small-scale mines, and where many people – including children – mine gold for a living. 
Read Richard’s story >>

SENEMA YA MAJAMBAZI NA POLISI DAR

ANGALIA PICHA ZA MAJAMBAZI WAKAMATWA NA POLISI BARABARA YA MANDELA BAADA YA KUIBA PESA KITUO CHA MAFUTA BUGURUNI MALAPA