Sunday, 14 November 2021

 TAARIFA KWA UMMA


Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya kiuongozi na kiutendaji ili kukidhi mahitaji ya wakati, mwenendo wa mabadiliko ya siasa za dunia na madhumuni ya Chama chetu katika kuwatumikia wananchi kikamilifu.

Hivyo Chama kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 32, waliobaki vituo vyao vya kazi ni 10, waliopangiwa vituo vipya ni 12 na wapya ni 9; aidha makatibu wa wilaya ni 168 ambapo waliopangiwa vituo vipya ni 67, waliobaki kwenye vituo vyao vya kazi ni 45 na wapya ni 56. Katika uteuzi huu kwa kuzingatia suala la jinsia wanawake ni 67 sawa na asilimia 33.5 na wanaume ni 133 sawa na asilimia 66.5.

Katika uteuzi huu hakuna hata mmoja aliyetoka nje ya mfumo wa Chama Cha Mapinduzi. Makatibu wapya wa Mikoa na Wilaya wametokana na kupandishwa hadhi  kwa makatibu wa CCM wa Wilaya, makatibu wa jumuiya za CCM Wilaya na Mikoa, Maafisa wa Chama na jumuiya Makao Makuu kwa utendaji kazi wao mzuri pamoja na makatibu waliorejeshwa kwenye utumishi kutokana na utiifu wao kwa Chama.

Katika uteuzi huu Kamati kuu ya Halmashauri kuu ilizingatia sifa za ziada ikiwemo uadilifu, uaminifu, weledi, uwezo, bidii, ubunifu, jinsia na rika. Makatibu wapya na waliohamishwa vituo vya kazi kwa Mikoa na Wilaya wanatakiwa kuripoti vituo vyao vya kazi mara baada ya kupokea barua zao. Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa na Wilaya uliofanyika ni kama ifuatavyo:-

Uteuzi huu umeanza mara moja kuanzia tarehe 6 Novemba, 2021.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, 
Itikadi na Uenezi.
8 Novemba,2021