Friday, 11 December 2015

ASKOFU CHARLES GADI AONGOZA UMOJA WA MAKANISA YA DODOMA KUMUOMBEA RAIS DK.JOHN MAGUFULI NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
 Viongozi wa Makanisa mbalimbali ya mkoani Dodoma wakiwa wameshika picha za Rais Dk.John Magufuli, Waziri Mkuu, Majaliwa Kasimu Majaliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu wakati wa kufanya maombi ya kuwaombea yaliyofanyika mjini Dodoma juzi. Maombi hayo yaliongozwa na Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry International la jijini Dar es Salaam.
 Viongozi hao na waumini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maombi hayo.
Picha ya pamoja ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wakati wa maombi hayo. Maombi hayo yalifanyika mjini humo baada ya viongozi hao na waumini mbalimbali kushiriki kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kuitumia siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru kufanya usafi nchi nzima.