Sunday, 24 November 2013


 Novemba 24,2013-Jumapili
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema, Zitto Kabwe Zubeiri anasema, licha ya hali ya kutoelewana ndani ya chama chake, hatojiondoa na kwamba hizo ni hisia tu za watu.
Ameweka bayana yamoyoni mwake leo Jijini Dar es Salaam alipoongea na waandishi wa habari na koongeza, "...kwa sababu watu wamezoea kwamba watu wakigombana, wasipoelewana ndani ya vyama, basi ni lazima mtu atoke ajiunge na chama kingine. Kwa hiyo Siondoki Chadema na ninaendelea kua mwanachama wa Chadema."
Mh.Zitto Kabwe(Kulia) Mbunge wa Kigoma Kaskazini akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo Jijini DSM, wakati akitoa taarifa yake kuhusu kuvuliwa nyadhfa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na aliyekuwa Makamu Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Kitilya Mkumbo(Kushoto pichani) katika Hoteli ya Serena Jijini hapa.

Mbunge huyo alisema ni jambo la kawaida kwa watu kutoelewana na kwamba kuna tofauti ya mitizamo ndani ya chama. Anasema kuna tofauti za mitizamo kuhusiana na suala la demokrasia ndani ya chama,kuhusu uwajibikaji ndani ya chama, kuna suala la kuheshimiana ndani ya chama lakini siyo tofauti za kumwezesha kukihama chama hicho.

Zitto anasema "sikujiunga mimi na Chadema labda kwa sababu nilikwenda kwenye kura za maoni za chama kingine nikakataliwa ndipo nikapata hasira na nikajiunga na Chadema, hapana. Nilijiunga na Chadema kutokana na kuamini misingi ya Chadema, walakini ni wazi kabisa kwamba ni lazima ifikiye wakati viongozi inapokua hamuelewani, ni lazima moja apishe nagfasi ya wengine watekeleze majukumu yao."
                        Pichani ni Dk Kilya Mkumbo naye akitoa yake ya Moyoni katika mkutano huo leo.

Zitto amesema ikiwa ataondoka, basi ataondoka kakutoka uwongozi lakini si uwanachama. Na anasema hamini nadharia ya kuhama chama, kama vile alivyo pinga kuhama kwa Thomas Kashilila na kujiunga na NCCR Mageuzi.