Thursday, 25 April 2013

 Wazee waasisi wa Temeke, wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, wakiwa wameambatana na ujumbe wa kumpongeza kwa utendaji mzuri hususan katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akizungumza na baadhi ya wazee waasisi wa Temeke, walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, leo kumpongeza kwa utendaji wake mzuri katika kubaini na kutanzua vitendo vya uhalifu hususani katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke, wazee hao waliongozwa na Kapteni mstaafu wa Jeshi Ndugu Mohamed Ligola.Picha na Demetrius Njimbwi- Jeshi la Polisi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Walioziwasilisha hati zao ni pamoja na Balozi Mpya wa Morocco nchini Tanzania  Mhe.Abdelilah Benryane,  Balozi mpya wa Hungary Mhe.Sandoz Juhasz,Balozi mpya wa Austria Mhe. Christian Hasenbichler  na Balozi Mpya wa Chille nchini Mhe.Konrad Paulsen.Pichani Balozi Mpya wa Morocco Mhe.Abdelilah Benryane akiwailisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Picha na Freddy Maro-IKULU
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Zitto Kabwe
--
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba 
“Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu. 
Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa. 
Ushauri- tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents” nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya  ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.