Friday, 30 December 2011

changa moto la maafuriko dar

Heshima yako Bwana Amani,
Mimi huwa mara nyingi nasita sana kuchangia hoja ambayo wanayoshiriki siwaoni au siwafahamu, maana nawafahamu wengi ambao wamekuwa very genuine katika kuchangia hoja katika msingi ya uzalendo na uchungu wa Taifa ambalo ni letu wote isipokuwa madaraka yake si yetu wote , hivyo unapotoa hoja inayokosoa walio madarakani, basi unakuwa umewapa sababu ya kukukandamiza. Ila nataka niamini kuwa wanaochangia hoja hii wengi wana uzalendo wa kweli kusaidian kupata 'constructive ideas' ambazo zitatusaidai kutoa muongozo stahili kwa swala ambal lisposhuglikiwa leo au kesho, keshokutwa maafa yake yatakuwa zaidi ya haya. Na ndiyo maana nadhani kuwa utamaduni unaojitokeza wa baadhi ya taasisi au vikundi kugawa nguo, sukari , au sabuni is simply trying to 'prescribe the wrong medication to a terminal disease'.
Nilikuwa nyumbani kipindi cha Bunge la Bajeti, nikamusikia Mh Anna Tibaijuka akitoa vision ya serikali kuhusu Bonde la Msimbazi, nadhani alikuwa anawaasa watu walioko kwenye bonde hilo wahame ili ligeuzwe kuwa mahala pa mapumziko(Gardens). Nakumbuka pia Mh Zungu wa ilalla nadhani akichangia hoja hii, alichangia hoja hii kwa jazba na, mchango wake haukujaribu kujenga hoja yoyote kati ya hizi tunazojaribu kujenga miezi mitano baada ya bajeti. Yeye aligeuza hoja kuwa campaign yake ya 2015, akafika kumwambia Mh. Tibaijuka, kuwa nanukuu ' Siungi mkono hoja, sis wakazi wa Dar Saaalama, biashara yetu kubwa ni nyumba, hatuna ziwa, au mazao kama nyie wa Kanda ya Ziwa, na Mikoa ya kati, na ndiyo maana mlikuwa wakali wakati wa bajeti ya Uchukuzi na Mawasiliano, sasa leo sie muntwambia tuhame bonde la msimbazi ili nyie mpate sehemu ya kuja kumpumzikia mkila koni, mimi niko tayari kuongoza maandamano kupinga hili wazo, maana hatuna maala pengine pa kwenda, hivyo nyie bakini huko huko mkila koni zenu, sisi tutakula ubuyu'
Nilijiuliza mambo mengi KM. Huyu mbunge ameongeza nini katika hoja hii? , Je ilifika fika je kuwa Wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na kati vs Dar es Salaam? Huyu bwana kwanini hakuhoji zaidi mambo ya msingi yaliosababishwa hoja hii ikaja bungeni, Je sera za serikali zinapobezwa kwa simple politics , nani anaumia.
Lakini jamani , mimi niko tayari kusimama popote to prove this bein said, maana katika picha zote sikumuona Huyu Mbunge among the victims, if they are really victims, na hatuwezi kudai ni victims wa sera mbovu za serikali , wakati zinapoletwa panapositahili kuhojiwa, kurekebishwa, na kufafanuliwa zaidi, waliopewa dhamana wanafanyia
siasa zisizo na tija.
Mimi nadhani, uwajibikaji ulitakiwa kuaanza na wabunge kama kina Zungu, walitakiaw baadala ya Kuchochea watu wasiondoke, wangetumia ubunge kufuatilia hilo swala Wizara husika, na sio cheap politics.
Mimi nina imani na hakika kuwa kwenye hoja ya serikali kwenye Bajeti, haya yote tunayoyahoji yatakuwemo, kama yamo, hakuna kisingizio kwa wanaoitwa 'victims' kuhama. Otherwise, inakuwa siyo serikali, tusishabikie kuwepo sheria na sheria kuchukua mkondo wake pale serikali inapojaribu kuzima upinzani wa mawazo na sera, bali hata pale inapojenga hoja na wanainchi wakakaidi kuitekeleza.
Nawasilisha Hoja!
JOHN LUSINGU