Friday, 15 April 2011

CHAMA CHA MAPINDUZI.

TAWI LA UNITED KINGDOM.

2 Apple Shaw Court, School Rd, Reading, RG31 5AL.

Katibu wa Tawi Direct Tel. +44 7799435327 or Email katibuwatawi@ccmlondonuk.org

Mwenyekiti wa Tawi Direct Tel +44 7900040288. Or Email owinoz@yahoo.co.uk

Website: www.ccmlondonuk.org E-mail: ccmlondon@gmail.com


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

PONGEZI KWA M/KITI WA CCM TAIFA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE NA WAJUMBE WAPYA WA KAMATI KUU, SEKRETARIATI NA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

Chama Cha Mapinduzi Tawi la UK kimefuatilia kwa makini na shauku kubwa vikao vya CCM Taifa viliyofanyika huko Dodoma hivi karibuni, na imeridhika na kukaribisha kwa dhati mabadiliko makubwa ya safu ya uongozi yaliyotokea katika Kamati Kuu, Sekretarieti na H/Kuu ya CCM Taifa.

WanaCCM wote waishio Uingereza, wanawapongeza viongozi wote ambao utumishi wao ulifanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu 2010, na sasa wamekubali kujiuzulu na kutii wito wa kuwajibika kwa manufaa na maslahi ya Chama.

CCM UK inatafsiri mabadiliko haya kuwa sio tuu ni uthibitisho wa kukomaa kwa demokrasia ndani ya Chama chetu, bali ni mfano wa Chama chenye siasa pevu zenye kuona mbali. Mabadiliko haya yanadhirihisha uwezo wa CCM kusimamia mabadiliko ya ndani na nje bila kutetereka, hasa wakati huu wa mabadiliko makubwa dunia.

CCM UK inaamini kuwa sababu za mabadiliko haya ya uongozi ni kuboresha utendaji kazi ndani ya chama kwa lengo la kuwatumikia kwa ufanisi zaidi watanzania wote.

Aidha CCM UK ina matumaini kuwa uongozi mpya utajifunza mbinu mpya na za kisasa za kisiasa kwa kuwasikiliza wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla na hivyo kutoa majibu madhubuti ya hoja zao na kupanga mikakati ya kukabiliana nayo na kwa mahitaji ya kizazi kipya na changamoto mpya.

CCM UK ina ahidi kuendelea kutoa ushirikiano unaostahili kwa uongozi mpya kwa manufaa na masalahi ya Chama Cha Mapinduzi na Taifa letu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA MUNGU IBARIKI TANZANIA.

12 April, 2011