Saturday, 7 February 2009



Africa Action & Howard University Department of African Studies

Presents

U.S. - Africa Policy "Projecting Change and Continuity
Under the Obama Administration"


Thursday, FEBRUARY 19
9:00AM-3:00PM

Howard University
Blackburn Center


The keynote address will be given by

Congresswoman Barbara Lee, followed by presentations by
experts on Africa in the Global Economy, Conflict and Militarism,
and Climate Change. See flyer attached.

To RSVP and for additional information please email OUTREACH@AFRICAACTION.ORG
or call 202-546-7961


Mjane wa Ntimbanjayo Millinga, Conrada Millinga pamoja na Yule Mwalimu wa kijiji mashuhuri kule Ruvuma kwa miaka ile ya 60, chini ya RDA, anategemea kutembelea Scotland baada ya kuhudhuria matukio kadhaa pale London, ikiwa ni pamoja na BTS na kutoa hotuba pale Ubalozi wa Venezuela.Ugeni huu utakuwa Scotland kuanzia Alhamisi hadi Jumapili wakati watakaporejea London kwa kujiandaa na safari ya nyumbani.Itakuwa vema sana tukiweza kuonana nao muda muafaka. Nikipata taarifa zaidi (kama wapi tutaweza kuonana nao rasmi na lini) nitazituma kwa wote kwa wale watakaoweza kuwa na nafasi.Kwa wale ambao hawafuatilia, Mwalimu Toroka na Mwalimu Millinga walikuwa ni wale waasisi wa mwanzoni kabisa kule Tanzania Ruvuma katika harakati za kijitegemea kwa hali halisi na mfumo wao uliweza kuwapa watu waliofanya nao kazi nguvu za kweli za kufanya maamuzi yao ya maisha yao ya kila siku. Waliweza kutimiza yote hayo kwa njia za kujadiliana, kusikilizana na pia kujishughulisha kwa mikakati dhabiti ya kujikomboa kisiasa na kiuchumi. Walifanya hayo chini ya RDA - Ruvuma Development Association. Wengi tunaojaribu kufuatilia hadithi nzima ya RDA, tunapata picha kuwa hizi juhudi ziliwatisha wengi wakati ule, haswa viongozi, kwani watu waliweza kufanya maamuzi mengi makubwa na ya maendeleo na kupunguza tegemezi kwa kiasi kikubwa kutoka Serikalini au kwa tabaka la viongozi. Huu ulikuwa ndio mwelekeo Mwalimu Nyerere alikuwa akiupigania. Cha kushangaza ni kwamba viongozi hao hao, chini ya kamati kuu ya chama, waliishia kutoa hoja ya kuvunja RDA na mwishowe RDA ilikuwa mwisho wake.Mengi yamendikwa, na yanaendelea kuandikwa juu ya hili. Kwa upande wetu sisi kama kizazi cha karne hii, naamini ni wajibu wetu kujua nini haswa kiliendelea kule, na pia kujifunza pale penye somo. Hakuna njia nzuri kama kuonana na kuongea na hawa waasisi. Kule nyumbani huwa tunakaa chini na wazee wanatupa hizi hadithi za huko awali. Huku ugenini, ni vema wakitokea tujaribu kukamata hiyo nafasi pale panapowezekana. Ingawa ni kibaba, ila wahenga walisema, kibaba kibaba hujazilia.Ndugu yenuApollo Temu