THE PRESIDENT OF ZANZIBAR H.E AMANI KARUME
RAIS Amani Abeid Karume, ametoa masharti ya kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu Muafaka na kumtaka kwanza amtambue kuwa ni Rais halali aliyechaguliwa kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2005.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Ikulu visiwani zanzibar baada ya kurudi safari ya Marekani, Rais Karume alisema kimsingi hana matatizo na Maalim Seif kukutana naye na kuzungumzia mustakabili wa kisiasa nchini,lakini amtambue kwanza kuwa ni Rais aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuongoza visiwa vya Unguja na Pemba."Milango iko wazi kwa mtu yeyote kukutana nami...hata ninyi waandishi wa habari si mnakuja hapa...lakini masharti ni lazima anitambue mimi kama Rais halali niliyechaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005," alisema Rais Karume.
Alisema hilo kutokana na swali aliloulizwa kuhusu moja ya masharti ambayo CUF inayatoa kwa sasa ili kuanza tena kwa mazungumo ya Muafaka wa kisiasa,kati ya vyama hivyo ambao kwa sasa unaonekana wazi kukwama.CUF wanataka ili kurudi katika meza ya mazungumzo ya Muafaka, Rais Jakaya Kikwete kwanza aingilie kati na kuwakutanisha Maalim Seif na Rais Karume, hatua ambayo itawezesha mazungumzo hayo kuanza tena baada ya kukwama.Habari hii na Ali Suleiman
REF[HAKI NGOWI]

Aliyekuwa gavana mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Timoth S. Ballali amefariki.Kwa habari zenye uhakika toka kwa ndugu wa karibu na mkewe,Mama Anna Muganda zinatonya kuwa amefariki Tarehe 16.05.2008 huko BOSTON, USA na anatarajiwa Kuzikwa ijumaa Boston Nchini Marekani.------------
Nyadhifa Alizoshika Enzi ya
Uhai Wake..
-Mwaka 1967-1976 alikuwa mtumishi katika Benki kuu ya Tanzania alishika nyadhifa mbalimbali.
-Mwaka 1979 -1984 alifanya kazi nchini nGhana akiwa kama mtumishi wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) kama mchumi.
-Mwaka 1984-1986 akiwa IMF alihamishiwa Zimbabwe katika nafasi hiyo ya mchumi.
- 1986-1997 aliongoza Timu ya IMF kwa ajili ya majadiliano na usimamizi wa sera ya mageuzi ya uchumi.
-1997-1998 aliteuliwa kuwa mshauri wa Rais wa mambo ya uchumi. na
Mwaka 1998 aliteuliwa Rasmi kuwa Gavana wa BoT,wadhifa aliodumu nao hadi Januari 2008.Kabla ya Rais Kikwete Kutengua uteuzi Bw Balali Mwezi January 2008.
Hat Hivyo wakati akiwa Gavana IMF ilimteua tena mwaka 2006-2008 kuwa mjumbe wa bodi ya Magavana akitokea Tanzania. Na mwaka 2006 alikuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato (TRA).

[ref.haki ngowi]
Is this the Price for Indipendence and self governance south Africa Style?