https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0kEsqOSrEuKjdDTtZT0DnY1tYrMFwEymIiLVy7RHgL0rWB_dbP7m9I46q7GEoDz56mR-DDyjUn9ljNjhOy6FEfXCo_utDtbAhfVk7des7o4ZsTyc0QmKA9S2LpvsId1-fbX46WEE0YaMj/s1600/IMG_5311.JPG" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg0kEsqOSrEuKjdDTtZT0DnY1tYrMFwEymIiLVy7RHgL0rWB_dbP7m9I46q7GEoDz56mR-DDyjUn9ljNjhOy6FEfXCo_utDtbAhfVk7des7o4ZsTyc0QmKA9S2LpvsId1-fbX46WEE0YaMj/s640/IMG_5311.JPG
" width="640" />
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania Salome Kitomari akienelea kutoa elimu juu ya waandishi wa kujua umuhimu wa kuendelea kusoma kwa kuwa elimu haina mwisho
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYVnTLqIpn_bQlPzH4NAKzzkdo1NhheT07gjQGBiK8gkx8OjTEvVTHmm6oceEwO45DI_mHNBy-tzcuJxX2w-XkqbK6YIZVHVG11AHDEuBs3KfMathWsjGxX6MWgKUVSquErvuRdt1yEye_/s1600/IMG_5348.JPG" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYVnTLqIpn_bQlPzH4NAKzzkdo1NhheT07gjQGBiK8gkx8OjTEvVTHmm6oceEwO45DI_mHNBy-tzcuJxX2w-XkqbK6YIZVHVG11AHDEuBs3KfMathWsjGxX6MWgKUVSquErvuRdt1yEye_/s640/IMG_5348.JPG" width="640" />
Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3H5DCrpE5a8sVx-qGcTyX86MJ2-r2D_kA0m8WusM1iBWfSbYLz8oOefUPteSzycOMnIQtEcC8KBhRHJarQG0L079eE1I516SaRa4NGPo4JpJjGeTezQZST2gRVnc7bqrSp846NE2EbvWR/s1600/IMG_5359.JPG" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3H5DCrpE5a8sVx-qGcTyX86MJ2-r2D_kA0m8WusM1iBWfSbYLz8oOefUPteSzycOMnIQtEcC8KBhRHJarQG0L079eE1I516SaRa4NGPo4JpJjGeTezQZST2gRVnc7bqrSp846NE2EbvWR/s640/IMG_5359.JPG" width="640" />
Waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa makini kusikiliza mjadala ambao ulikuwa unaendelea kuhusu umuhimu wa elimu ya uandishi wa habari
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjz2vGpcCCa8VSsGtqpaUFms4lREZas7xw79AXV68eLlBinc9Dih1LPGITJSWztXZVjtCjKv0bTaH6WwTlfMzb3oiCywxCnvHtn18QGuwx4vgbWqvliEZ5CivPXNmcbCVHQ_0KmZbUYNchU/s1600/IMG_5375.JPG" imageanchor="1" style="margin-left: 1em; margin-right: 1em;">https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjz2vGpcCCa8VSsGtqpaUFms4lREZas7xw79AXV68eLlBinc9Dih1LPGITJSWztXZVjtCjKv0bTaH6WwTlfMzb3oiCywxCnvHtn18QGuwx4vgbWqvliEZ5CivPXNmcbCVHQ_0KmZbUYNchU/s640/IMG_5375.JPG" width="640" />
Waandishi wa habari na wadau wa habari wa mkoa wa Iringa wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa MISA Tanzania
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wanahabari mkoa wa Iringa wametakiwa kuongeza
kiwango cha elimu ili kuweza kufanya kazi kwa kujiamini na kwa weledi wa hali
ya juu katika kazi zao.
Akizungumza kwenye majadiliano ya kubaini
changamoto za waandishi wa habari mkoani Iringa mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo
vya Habari Kusini mwa Africa (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na
Internews,Salome Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari mkoani Iringa
wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi kutokana na elimu uliyonayo.
“Waandishi wakiwa na elimu ya uandishi wa
habari wanapaswa kuishi maisha yaliyo mazuri kwa manufaa ya jamii kwa kuwa
waandishi wa habari ni kioo cha jamii,mwandishi unapaswa kujiuliza kwenye jamii
unaonekanaje kutokana na kazi yako” alisema Kitomari
Kitomari alisema kuwa waandishi wa habari
wanatakiwa kuwa nadhifu muda wote kutokana na taaluma inavyotaka ili kuweza
kutambulika kisheria kama taaluma nyingine ambazo zinatambuliwa vizuri kwa
muonekano wao kwa wanataaluma wao.
“Waandishi wa habari mnatakiwa kuvaa mavazi
nadhifu kama ilivyo wanasheria ambavyo wamekuwa wanaonekana wawapo kazini ndio
maana wanaaminika zaidi ya waandishi wa habari hivyo inatupaswa kubadilika
kimuonekano” alisema Kitomari
Aidha Kitomari alisema ikifika 2021 kama huna
elimu ya stashada ya elimu ya uandishi wa habari hautakuwa na fursa ya
kuendelea kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa mujibu wa sheria za nchi hii.
“Kama
ujaanza kusoma stashada ya elimu ya uandishi wa habari basi ikifika 2021
utakuwa hujamaliza hivyo hutakuwa na sifa za kuwa mwandishi wa habari hasa
usisubili changamoto hiyo ikukute jiongeze kitaaluma.” Alisema Kitomari
Lakini katika majadiliano ya kubaini changamoto
kwa waandishi wa habari mkoani Iringa kuliibuka changamoto kama tatizo la
uchumi kwa mwandishi mmoja mmoja ambapo ilionekana waandishi wengi hawaandiki
habari kiweledi kutokana na na tatizo la kiuchumi.
Raymond Minja mwandishi wa gazeti la Mtanzania
alisema kuwa waandishi wengi wa sasa wamekuwa wakiandika habari za kusifu na
kuabudu kutokana na tatizo la uchumi kwa kuandika kile kitu anachokita mtoa
habari.
“Tunaandika sana habari za kusifu na kuabudu
kutokana na waandishi wengi kuwategemea watoa habari ambao mara nyingi wanakuwa
viongozi wa kada mbalimbali na kupelekea kutoka katika misingi ya taaluma ya
uandishi wa habari” alisema Minja
Waandishi wa habari wanachuki wao kwa
wao,hawapendani na wanaubinafsi kutokana na tatizo la changamoto ya uchumi duni
hiyo kupelekea waandishi wengi kuanza kutoka kwenye weledi wa taaluma hiyo,
alisema Denis Mlowe mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima