Thursday, 18 February 2016

JUKWAA LA BIOTEKNOLOJIA LATOA MAFUNZO KWA WALIMU WANAFUNZI WA CHUO CHA BUNDA KUHUSU BIOTEKNOLOJIA
Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania na Mkufunzi wa Mafunzo ya Bioteknolojia , Dk.Emmarold Mneney (kulia), akiwafundisha wanachuo wa Chuo cha Ualimu cha Bunda (BUNDA TTC), kuhusu matumizi ya bioteknolojia na uhandisi jeni Wilaya ya Bunda mkoani Mara leo asubuhi.
Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wanachuo hao katika mafunzo hayo.
Wanachuo hao wakifuatilia mafunzo hayo. 


Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Rweyemamu wakiwa katika mafunzo hayo.
Walimu wa chuo hicho wakifuatilia mafunzo hayo.
Wanafunzi wakiwa katika mafunzo

Wanachuo hao wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo
Mwanachuo, Noshad Bryson akiuliza swali katika mafunzo hayo.
Mwanachuo, Mahana Mahana akiuliza swali.
Mwanachuo, Elias Yohana akiuliza swali.
Hapa baada ya mafunzo ni msosi kwa kwenda mbele.

Na Dotto Mwaibale

JUKWAA la Bioteknolojia Tanzania limetoa mafunzo ya matumizi ya bioteknolojia na Uhandisi Jeni kwa wanachuo cha ualimu Bunda kilichopo mkoani Mara ili kuwa jengea uwezo wa kuielewa teknolojia ya bioteknolojia  kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na changamoto za kilimo.

Akizungumza na wanafunzi hao jana Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Emmalord Mneney alisema kuwa teknolojia hiyo mpya ni muhimu kusambaa nchini ili kumkomboa mkulima.

"Tumeamua kuleta mafunzo haya kwa wanachuo hiki tukiamini kuwa baada ya kuhitimu mafunzo yao watakwenda kuwaelimisha wakulima katika maeneo yao"alisema Dk. Mneney.


Dk.mneney aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya tabianchi kumesababisha ukame na uharibifu wa mazingira ambayo yameathiri shughuli za kilimo hasa mazao.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali imekuwa ikiiwezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kwa ajili ya kuwaongezea uwezo wa kufanya tafiti za kilimo nchini.

Dk.Mneney alisema kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni kukosa mbegu bora za mazao ya pamba na mahindi hali iliyosababisha wakulima wengi kukata tamaa ya kilimo hicho na kuamua kulima mazao mengine.

"Kutokana na changamoto hiyo Costech imekuwa ikifanya utafiti ndani ya maabara ya kisasa iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ili kupata mbegu bora ambazo zikionekana kuwa zinafaa zitasambazwa katika mashamaba makubwa na nchi nzima kwa ujumla" alisema Dk.Mneney.


Mwanachuo hicho Mahana Mahana alisema mkoa wa Mara unachangamoto kubwa ya kilimo kutokana na ardhi kuchoka hivyo ni wakati wa watafiti kuliangalia hilo ili kuwasaidia wakulima kupata mbegu bora zitakazo waletea mafanikio ya kilimo ya kupata mazao mengi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)