Wadau Husni na Benedict Mponzi wakiwa katika pozi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita |
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Tigo Bw, Shavkat Berdiev akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita |
Wageni rasmi wakipiga ngoma kama kuashiria uzinduzi rasmi w a Intaneti ya kasi zaidi nchini ya TIGO 4G lte katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita |
Mgeni rasmi Wilson E Nkambaku , mkuu wa wilaya Arumeru akitoa hotuba fupi katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita |
Umati wa wakazi wa jiji la Arusha wakifurahia jambo katika katika hafla ya uzinduzi wa intaneti ya kasi ya Tigo LTE iliyofanyika jijini Arusha mwishoni wa wiki iliyopita |
Arusha,
Novemba 18 2015. Wateja wa Tigo waishio Arusha
sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia
upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo
kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano
zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es
Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkuu wa Kitengo cha Internet
David Zacharia.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Arusha, Zacharia amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo
imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha
ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya
kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi
na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandao wa
intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma
hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na ubora hali ya juu na kufanya
mikutano kwa njia ya mtandao.
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Arusha kwamba sasa
wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na Intaneti
yenye kasi zaidi,” Gutierrez amesema. Arusha ni makao makuu ya taasisi nyingi
za kimataifa ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki na kitovu cha utalii nchini.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE watanufaika na
promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama
bonasí.
Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza
kupatikana hivi karibuni kuwa ni Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza
na Tanga, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G
nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufkisha huduma ya 4G katika kila kona za
nchi ifikapo mwaka ujao, Zacharia ameongeza kusema.