--
-----------------------
Kituo cha Mtandao wa kijamii cha Mbeya Yetu (http://www.mbeyayetu.blogspot.com/" style="color: #1155cc;" target="_blank">www.mbeyayetu.blogspot. com
Msaada wa kwanza ulipokelewa hivi karibuni wenye thamani ya shilingi Laki Moja kutoka Familia ya Masawe wa Dar es salaam kwa ajili ya kituo cha Nuru ambapo Mbeya yetu iliuwasilisha kama ulivyo.
Mbali na msaada huo pia Mtandao huu ukishirikiana na mtandao wa kijamii wenye makao yake makuu Jijini Dar es salaam wa http://www.michuzi.blogspot.com/" style="color: #1155cc;" target="_blank">www.issamichuzi.blogspot.com
Aidha katika kuonesha wengi wameguswa na tukio la Mwanamke huyo kujifungua watoto wanne ambao wanaendelea vizuri, pia Msamaria mwema mwingine aliyejulikana kwa jina la Dada https://www.facebook.com/norah.silverboutique" style="color: #1155cc;" target="_blank">Norah SilverBoutique
Shukrani kwa Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza na ofisi za Michuzi Media Group (MMG) kuwezesha kufika kwa mizigo hii Mbeya.
Kutokana na kupokelewa kwa mizigo hiyo ambapo kituo cha Nuru kilikabidhiwa Katoni Mbili za Sukari, Sabuni na Biskuti pia Tunatarajia kuanza safari ya kwenda huko Chiwanda Wilaya ya Momba Kilomita zaidi ya 260 toka Mbeya mjini kufikisha misaada ya Mama wa mapacha wanne.
Hivyo ni wito wetu kwenu kuendelea kutuombea na kutuunga mkono katika safari hiyo ili tuweze kuifikisha salama mizigo hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia maendeleo ya Watoto hao ambapo watakuwa wameshatimiza mwezi mmoja na siku 24.
Tunawashukuru sana tena sana wote mliojitolea na Mungu awabariki sana.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com" style="color: #1155cc;" target="_blank">issamichuzi@gmail.com
Nasi tutafikisha ubani wako.
Wazee wa Kazi Serengeti Freight wametoa ofa ya
kusafirisha bure misaada ya aina hii toka Uingereza.
Mbarikiwe sana Wazee wa Kazi.