Thursday 9 August 2012




CHADEMA  WAVURUNDA KWA AIBU LONDON.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo jana kilipata AIBU kubwa hapa jijini London baada ya Watanzania kuzira kuhudhiria mkutano wao uliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.
Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa. Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.
Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya  watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo  Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.
Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI  FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha  mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda  kibichi.
Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha  ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.
Katika mahudhurio hayo machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja...wanafikiri hapa ni walipotoka..ovyoo.”
Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.
Na Rukia Kilemile 
Mwandishi wa kujitegea na mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United Kingdom.
Mwandishi si mwana chama wa chochote cha siasa.