Friday, 14 September 2012


Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais, aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama Britain Tanzania Society (BTS).

Leo hii siku ya Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, Mheshimiwa Makamu wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY

Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.

Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya Alhamisi tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe



Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif alikutana na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London. 
Katikati ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda, Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa Joan Rwabyomere (Pili kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa Bernard Ntahiraja (Kwanza kulia).





Makamu wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa Makamu wa Rais ni Bwana  David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi linalotolewa na BTS,  Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-  Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.