CHADEMA WAVURUNDA KWA AIBU LONDON.
Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo jana kilipata AIBU kubwa hapa jijini London baada ya Watanzania kuzira
kuhudhiria mkutano wao uliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The
Thatched House.
Sababu nyingi
zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala
cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa
sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa.
Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania
wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku
wakiacha mali zao nyuma.
Maandalizi ya mkutano
wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa
yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia
za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania
wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati
iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au
isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili
la rafiki zao Conservative.
Aidha waandaaji wakuu
wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na
usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti
imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania
kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya
Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji
au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda
uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.
Baadhi ya Watanzania
waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar
hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi
na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine
wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.
Katika mahudhurio hayo
machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine
kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na
kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja...wanafikiri
hapa ni walipotoka..ovyoo.”
Ikitarajia kufuata
nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na
si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi.
CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.
Na
Rukia Kilemile
Mwandishi
wa kujitegea na mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi
hapa United Kingdom.
Mwandishi si mwana chama wa chochote cha siasa.