Monday, 25 June 2012


 Bwana Gulfraz, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa kabla ya makabidhiano ya msaada wa Vifaa vya mchezo kwa Timu ya Cricket ya Tanzania.
 Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa (tatu kushoto), akipokea msaada wa Vifaa vya mchezo wa Cricket kwa Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Cricket ya Totteridge Millhill, Bwana Stewart Wenham (kwanza kushoto). Msaada huo wa Vifaa vilikabidhiwa kwa Mkurugenzi, Bwana Kashangwa, ni moja ya ushirikiano mzuri uliopo baina ya Timu ya Tanzania ya mchezo wa Cricket, Shirikisho la mchezo huo hapa Uingereza na Timu ya Cricket ya Watford. Wengine pichani ni maafisa wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.
--
Timu ya Cricket ya Watford ikiongozwa na Bwana Gulfraza Riaz, imekuwa ushirikiano wa karibu na Timu yetu ya Taifa ya mchezo wa Cricket, Tanzania, vile vile timu hiyo imekuwa mstari wa mbele kuitangaza Tanzania katika mchezo huo hapa nchini Uingereza, pamoja na kuandaa michezo ya majaribio kwa Tanzania kila mara.