MWENGE OH MWENGE MBIO MBIO
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) akiwasha mwenge wa uhuru kuashiria kuanza kwa mbio za mwenge huo kwa mwaka 2012 leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. Mwenge huo utakimbizwa kwenye jumla ya Halmashauri za wilaya, Manispaa na miji 157 na kuongozwa na kauli mbiu ya Sensa ya watu na Makazi ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo yetu Shiriki kuhesabiwa Agosti 26.
iongozi wa mbio za Mwenge Mwaka 2012, Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es salaam akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda tayari kwa kuukabidhi kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya tayari kwa kukimbizwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara (kushoto) akimtambulisha kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2012 Kepteni Honest Erenest Mwanossa kutoka Dar es salaam (kulia).