Ujumbe wa Tanzania (Kulia) ukiongozwa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda wakiwa katika kikao maalum na ujumbe wa Bunge la Japan (kushoto) uliongozwa na Mwenyeji wake Spika wa Japan Mhe. Takahiro Yokomichi. Mhe. Makinda yupo Japan kwa mwaliko maalum na Bunge la Japan kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi ya picha yenye wanyama (the Big Five animals) Spika wa Bunge la Ushauri la Japan (President of House of Councilors) Mhe. Kenji Hirata wakati alipo mtembelea Ofisi kwake baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Ujumbe wa Bunge la Japan na Tanzania leo kilichojadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya mabunge haya
Ujumbe wa Bunge la Tanzania ukiongozwa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya Bunge la Japan na ujumbe wa Bunge la Japan ambao uliongozwa na Mwenyeji wake Spika wa Japan Mhe. Takahiro Yokomichi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja kilichojadili namna ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya Mabunge ya Nchi hizi Mbili.