Sunday 30 September 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akiwa na Balozi Getrude Mongella kabla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe. NA DANIEL MBEGA, KISARAWE SPIKA wa zamani wa Bunge la Afrika, Balozi Getrude Ibengwe Mongella, amemtabiria mambo makubwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akisema kwamba anaamini atafika mbali katika uongozi wa nchi hii.