Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Tigo wa duka jipya la Tigo Tunduma mara baada ya ufunguzi wa duka hilo
Kampuni ya simu ya Tigo
imefungua duka jipya Tunduma ambalo limepunguza adha kwa wateja wa kampuni hii
ambao walikuwa wanatafuta huduma kwa wateja umbali mrefu toka kwa makazi yao
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa duka hilo Mkurungezi wa Tigo Kanda ya kusini Bw.Jackson Kiswaga
alisema uzinduzi wa duka hili ni moja ya mipango ya kampuni ya Tigo kusogeza
huduma karibu na wateja wake.
"Kampuni ya tigo imeangalia fursa zilizopo katika
eneo la Tunduma ambapo kwa pamoja tumeiona ni jinsi gani tunaweza kusaidiana na
wakulima na wafanya biashara kuweza kufanya huduma mabalimbali za kibenki kwa
kutumia simu za mkononi"Alisema Kiswaga.
Kiswaga alisema kuwa duka
hilo linategemea kuhudumia wateja wapatao mia tatu kwa siku wakipata huduma
mbalimbali ikiwemo huduma za kuunganishwa kwenye intaneti, usajili wa laini za
simu na kurudisha laini zilizopotea pia kununua simu za kisasa.
Kwa upande wa katibu wa
mkuu wa wilaya ya Tunduma Mhe. Richard Mbeho alipongeza hatua za Tigo za
ufunguzi wa duka hili kwa kuwa utarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja wa
wilaya ya Tunduma.
|