
 Wazee waasisi wa Temeke, 
wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema,
 walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, 
wakiwa wameambatana na ujumbe wa kumpongeza kwa utendaji mzuri hususan 
katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP 
Said Mwema, akizungumza na baadhi ya wazee waasisi wa Temeke, 
walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Dar es salaam, leo 
kumpongeza kwa utendaji wake mzuri katika kubaini na kutanzua vitendo 
vya uhalifu hususani katika mkoa wa Kipolisi wa Temeke, wazee hao 
waliongozwa na Kapteni mstaafu wa Jeshi Ndugu Mohamed Ligola.Picha na 
Demetrius Njimbwi- Jeshi la Polisi

Rais
 Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa 
mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa.Walioziwasilisha hati zao 
ni pamoja na Balozi Mpya wa Morocco nchini Tanzania  Mhe.Abdelilah 
Benryane,  Balozi mpya wa Hungary Mhe.Sandoz Juhasz,Balozi mpya wa 
Austria Mhe. Christian Hasenbichler  na Balozi Mpya wa Chille nchini 
Mhe.Konrad Paulsen.Pichani Balozi Mpya wa Morocco Mhe.Abdelilah Benryane
 akiwailisha hati zake za utambulisho kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
 ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Picha na Freddy Maro-IKULU
Apr
24

Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema. Zitto Kabwe
--
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba 
“Moja,
 mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie 
najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi 
hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu. 
Pili,
 hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. 
Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama 
yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. 
Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake 
litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya 
Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka 
zitachukuliwa. 
Ushauri-
 tuwe makini na “Agente provocatuers” au in English “provocation agents”
 nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against 
provocations. Nadhani mmenipata”
Nawatakia
 Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja 
na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini na ugandamizaji.
Majibu haya  ameandika kupitia mtandao wa Kijamii wa facebook.