JIMBO LA UCHAGUZI-KIGOMA KASKAZINI
08.11.2012
.jpg)
Rais Jakaya Kikwete Akiwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma Leo

Rais
 Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Nape 
Nnauye Muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete Kuwasili Mkoani Dodoma 
leo  tayari kuongoza vikao na mkutano mkuu wa nane wa CCM
Nov
9

Jumuiya
ya watumiaji wa huduma mbalimbali nchini kupitia mitandao ya kijamii ya
Facebook na Twitter imezindua rasmi shindano la kusaka kampuni zinazotoa huduma
na bidhaa mbovu kwa wateja nchini Tanzania. 
Jumuiya
hiyo inawajumuisha watu wa kada mbalimbali wakiwemo wanasheria, wanaharakati,
waandishi wa habari, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wateja wa huduma
na bidhaa mbalimbali nchini Tanzania.
Lengo
la jumuiya hiyo ni kushinikiza wafanyabiashara nchini kutoa huduma na bidhaa
bora kwa wateja na kuwakumbusha umuhimu wa wateja. Kauli mbiu ya wanajumuiya
hao ni Mteja ni Mfalme.
Katika
wiki ya kwanza tangu jumuiya hiyo kuzinduliwa jumla ya makampuni 21 yameingizwa
katika shindano hilo kwa wateja wao kuwasilisha malalamiko yao. Kwa taarifa
zaidi kuhusu ni fuatilia akaunti ya Twitter @hudumambayatz au kundi la Facebook linalojulikana kama HUDUMA BONGO.
Ili
kuweza kupiga kura yako unahitajika kuwa na akaunti hai (yenye mawasiliano mara
kwa mara) katika mtandao wa Twitter au Facebook na kujiunga na jumuiya hiyo. Mara
tu utakapowasilisha kero yako utaifanya kampuni unayoilalamikia kuingia katika
mchuano mkali wa kumsaka bingwa wa huduma mbovu kwa wateja nchini. 
Huduma
Bongo inatoa wito kwa makampuni yote kuboresha huduma na bidhaa zao ili kuweza
kuwapatia wateja kilicho bora zaidi katika soko hili la ushindani.
Imetolewa na 
Mshauri wa
Habari wa Huduma Bongo 
Novemba 9, 2012 
Nov
9



 Barabara za katikati ya mitaa ya manispaa ya Dodoma zikiwa zinatengenezwa kwa kiwango cha Lami.
Wajasiriamali
wakiwa wameweka biashara zao kwenye moja ya mageti ya makao makuu ya
CCM,kipindi hiki cha mkutano mkuu kumekuwa na maongezeko ya mahitaji ya
bidhaa za chama bora Tanzania,hivyo kutoa fursa kwa wafanya biashara
wengi kuuza bidhaa za chama hicho.Picha na Adam Mzee-Dodoma
Nov
8

Mkurugenzi
 wa Kampuni ya Best Import Zanzibar  Issa Kassim Issa kushoto 
akimkabidhi Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali 
Abadallah dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya kusaidia matibabu ya 
Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga katika Ofisi ya Makamo wa 
Pili wa Rais Vuga mjini Zanzibar.Picha na Yussuf Simai Maelezo Zanzibar.
--- 
Na : Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 
Kampuni
 ya Best Imports Zanzibar inayojishughulisha na biashara ya uuzaji Kuku 
(Paja Nono) imetoa jumla ya Dola 2000 za kimarekani kwa ajili ya 
kusaidia matibabu ya Katibu wa Mufti Zanzibar Skeikh Fadhil Soraga.
Akitoa
 msaada huo leo kupitia kwa Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais 
Zanzibar,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Issa Kassim Issa amesema wameamua 
kutoa mchango huo kutokana na kuguswa na kitendo cha kinyama 
alichofanyiwa Sheikh Soraga na kwamba kiasi hicho cha pesa kitatumika 
kusaidia matibabu yake.
Issa
 amesema wamiliki wa Kampuni hiyo David Aloy na Carlos Ajala wamestushwa
 na kitendo alichofanyiwa Sheikh Soraga ambaye ni mtu muhimu katika 
jamii kutokana na mchango wake mkubwa.
Ameongeza
 kuwa Shekh Soraga ni mtu mwenye heshima kubwa Zanzibar kutokana na 
shughuli zake za kila siku na kwamba kitendo alichofanyiwa kinapaswa 
kulaaniwa na kila mtu.
Kwa
 upande wake Katibu wa Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Abadallah Ali 
Abadallah aliishukuru Kampuni hiyo kwa kuwa wa kwanza kutoa msaada wa 
kifedha na kuahidi kiasi hicho cha fedha kitapelekwa sehemu husika.
Aidha
 Katibu huyo amewaomba wananchi kumuombea Shekh Soraga apone haraka na 
wale wenye uwezo kuiga mfano wa Kampuni ya Best Import ili kufanikisha 
matibabu hayo.
Sheikh Soraga ambaye anatarajiwa kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi ameumia sehemu za usoni,mikononi na kifuani  baada
 ya kumwagiwa Tindikali na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akifanya 
mazoezi viwanja vya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi Unguja.
Nov
8
ZANZIBAR ALHAMISI NOVEMBA 8, 2012.
 Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Kisiwani Zanzibar wanaotuhumiwa kwa
 makosa tofauti ya kutoa lugha za uchochezi na kusababisha ghasia na 
vitendo vya uvunjifu wa amani uliopelekea uharibifu wa miundombinu ya 
barabara ambao leo walifikishwa Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar, 
wamerudishwa tena Rumande.
Kesi hiyo ambayo inawakabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar iliitwa mahakama kuu kwa kutajwa baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Hata hivyo, kabla ya kutajwa tena kwa kesi hiyo, huku kukiwa na ulinzi mkali wa Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ndani ya Mahakama hiyo kulizuka mabishano makali ya kisheria huku kila upande ukionyesha ujuzi wao wa kisheria.
Kwa upande wa Mawakili wa Watuhumiwa Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma Kaka, wakiwasilisha hoja mbalimbali za uvunjifu wa haki za watuhumiwa ikiwemo ya kunyolewa ndevu wakiwa Rumande katika Chuo cha Mafunzo jambo ambalo ni kinyume na uhuru wa kuabudu kwani wamesema ndevu kwa mashehe ni sehemu ya ibada.
Baada ya kuwasilisha hoja hizo, Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ramadhani Nassibu, akinukuu vifungu vya sheria vilivyopo kwenye Katiba ya Zanzibar na kusema kuwa kama kuna haki zinazovunjwa na chombo chochote ama mtumishi wa Serikali kuna mahala pengine pa kupeleka malalamiko hayo.
Baada ya mabishano hayo, Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi, aliamuru watuhumiwa wote warudishwe tena rumande hadi Novemba 20, mwaka huu itakapokuja tena katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kutajwa.
Kesi hiyo ambayo inawakabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar iliitwa mahakama kuu kwa kutajwa baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Hata hivyo, kabla ya kutajwa tena kwa kesi hiyo, huku kukiwa na ulinzi mkali wa Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ndani ya Mahakama hiyo kulizuka mabishano makali ya kisheria huku kila upande ukionyesha ujuzi wao wa kisheria.
Kwa upande wa Mawakili wa Watuhumiwa Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma Kaka, wakiwasilisha hoja mbalimbali za uvunjifu wa haki za watuhumiwa ikiwemo ya kunyolewa ndevu wakiwa Rumande katika Chuo cha Mafunzo jambo ambalo ni kinyume na uhuru wa kuabudu kwani wamesema ndevu kwa mashehe ni sehemu ya ibada.
Baada ya kuwasilisha hoja hizo, Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ramadhani Nassibu, akinukuu vifungu vya sheria vilivyopo kwenye Katiba ya Zanzibar na kusema kuwa kama kuna haki zinazovunjwa na chombo chochote ama mtumishi wa Serikali kuna mahala pengine pa kupeleka malalamiko hayo.
Baada ya mabishano hayo, Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi, aliamuru watuhumiwa wote warudishwe tena rumande hadi Novemba 20, mwaka huu itakapokuja tena katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kutajwa.
 
Na
 Mohammed Mhina,
Jeshi la Polisi Zanzibar
Nov
8

Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe- (MP), Tanzania Minister for Transport  
---  
Britain Tanzania 
Society (BTS) Annual general meeting will be held at  Westminster Central Hall, Saturday 10 November 2012, 
starts at 2PM. Hon. Dr. Harrison G. Mwakyembe- (MP), Tanzania Minister for Transport - guest speaker, will be talking on "The Quest for a New Constitution 
in Tanzania: Prospects and Challenges".
The next BTS Seminar is at SOAS on December 
6th at 5PM, on the media and democracy in Tanzania.
Malaika Kids, a childrens charity familiar 
to many of you, is having it's annual London reception on November 20th 
from 6-8.30PM at 120 Moorgate,and BTS members are welcome to attend.  
Also, there are fascinating article on the 
BBC website recently about the spread of the internet in Tanzania, which 
might well be of interest.  The pace of change is quite extraordinary.  

 
U.S. Ambassador to Tanzania 
Alfonso E. Lenhardt (right), present's ambulance keys to the Chief of 
Medical Services of the Tanzania Peoples Defense Force (TPDF), Major 
General AS Mwabulanga, (left), during a donation ceremony held yesterday
 at the TPDF Headquarters in Dar es Salaam.

US Ambassador to Tanzania, Alfonso
 E. Lenhardt, (fourth from right), Chief of Medical Services of the 
Tanzania Peoples Defense Force (TPDF), Major General AS Mwabulanga, 
(fourth from left) following the donation ceremony by the United States 
yesterday at the TPDF Headquarters in Dar es Salaam. Others officials 
pictured are Country Director, Walter Reed Army Institute of Research  
(WRAIR),  Edward Sekonde, (right); Master Chief, Operations Coordinator,
 Defense Attaché Office, Vladimir T. Narvaez, (second from right); 
Brigadier General LS Msangi, (third from right); and Colonel DB Maganga,
 (left); Senior Defense Official/Defense Attache, Lieutenant Colonel, 
Kevin C. Balisky, (second from left); and General Officer Command of 
General Military Hospital Brigadier General VT Lyimo, (third from left).
  
Nov
8

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la
 gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno 
ya Kinyerezi njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt 
Mohamed Ghalib Bilali.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed 
Ghalib Bilali na viongozi wengine wakimsikiliza  Waziri wa Nishati na 
Madini Profesa Sospeter Muhongo miundombinu ya  bomba la gesi asilia 
toka Mtwara hadi Dar es salaam leo Novemba 8, 2012 maeneno ya Kinyerezi 
njijini Dar es salaam. Nyuma yake ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib 
Bilali.

Rais
 Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba 
la gesi asilia kutoka Mtwata hadi Dar es salaam, Benki ya Exim ya China 
na viongozi waandamizi wa serikali alipowakaribisha Ikulu kwa mazungumzo
 baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi 
jijini Dar es salaam.Picha na IKULU

