RAMADHANI MUBARAK
BIRMINGHAM RAMADHAAN EVENT 
LONDON RAMADHAAN EVENTS 
 | ||
HISTORIA YA SHILOLE
PICHA ZINAZOONESHA UOKOAJI UKIFANYIKA BAHARINI KUOKOA WAHANGA WA MELI YA MV SKAGIT...!
HIZI NI PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU MELI YA MV SKAGIT MIILI 24 IMEPATIKANA HADI SASA ...!
HAWA NI BAADHI YA WATU WALIOKUWEPO PEMBEZONI MWA ENEO AMBAPO WATU WATU 
WANAO OKOLEWA KUTOKA KWENYE MELI WANA WEKWA ILI HATUA NYINGINE ZIFUATWE.
HAWA NI BAADHI YA ASKARI WAKIWA KWENYE ZOEZI LA KUWAOKOA WAHANGA KATIKA MELI ILIYOZAMA JANA.
SUMATRA:MELI YA MV SKAGIT ILIKUWA NA ABIRIA 248, WATOTO 31 NA MABAGHARIA 9...!

MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na maji (SUMATRA),imesema meli ya MV Skagit iliyopata ajali visiwani Zanzibar, iliondoka Bandari ya Dar es Salaam saa 06.05 mchana juzi ikiwa na abiria 248, watoto 31 pamoja na mabaharia 9.
Meli hiyo 
inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport, ilipata usajili katika 
Mamlaka ya usafiri  Bandari Zanzibar (ZMA)ikiwa na uzito wa meli 
(GRT)96.
Akizungumza
 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Meneja Mawasiliano 
David Mziray, alichanganua kuwa cheti cha ubora wa meli hiyo kilitolewa 
Agosti mwaka jana na kumalizika mwezi huo mwaka huu.
“Mv Skagit
 ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26,  hivyo 
kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho 
isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria 
njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Mziray.
Aidha, 
anafafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha hadi sasa ni zaidi ya 
34, majeruhi 146 wakati wengine wakiendelea kutafutwa.
“Zoezi la 
uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa msaada wa Mv Flying Horse, 
Mv Kilimanjaro 111, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM, Mv Zanzibar 1, Polisi
 wa majini, pamoja na Navy, hata hivyo bado taarifa sahihi za 
waliopoteza maisha hazijapatikana kulingana na watu hao kuokolewa katika
 mazingira tofauti” alibainisha Mziray.

