Saturday, 9 October 2010


Ukoo wa Chuwa uliopo Stockholm SWEDEN, Unapenda kuwataarifu ndugu na jamaa wote kwamba Mazishi ya MONICA HANSSON CHUWA yatafanyika Jumatano ya tarehe 13/10/2010 saa 10:00 AM (Asubuhi) kwenye makaburi ya SKOGSKYRKOGĂ…RDEN "heliga kapel" SANDSBORG. Baada ya shughuli za mazishi ndugu na jamaa wote tutajumuika kwa pamoja kwenye ukumbi uliopo SKARPNĂ„CKS ALLE 33-35 kwaajili ya rambirambi.
Ukoo wa Chuwa unachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliojitokeza na waliotoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha shughuli hii ngumu ya msiba.
Tunawasisitiza wale wote watakaokuwa na nafasi wajitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuusindikiza mwili wa ndugu yetu mpendwa MONICA.
Kwa niaba ya Ukoo wa CHUWA,
FRED ZG SSEBUYOYA.