Footballer  Samuel  Etoo in  TanzaniaAJALI YA NDEGE TANZANIA

TAARIFA  KWA VYOMBO VYA 
 HABARI.
 --------
 Rais Jakaya Kikwete leo Juni 11, ameongoza waombolezaji katika  kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu waliofariki dunia katika ajali ya  helikopta ya jeshi iliyotokea Jumatatu wiki hii mkoani Arusha.
  Miili ambayo iliagwa rasmi ni ya rubani wa helikopita hiyo  Kanali Wakete, msaidizi wa rubani Meja Sinda, rubani msaidizi na fundi ndege  Luteni Kirunga pamoja na Bibi Irene Nkamba Jitenga, mke wa Brigadia Jenerali  Jitenga ambaye ndiye mkuu wa vikosi vya JWTZ kanda ya kaskazini.
  Rais Kikwete alikwenda kuaga miili hiyo mara baada ya kuwasili  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mapema asubuhi akitokea mjini  London Uingereza ambako alihudhuria kikao cha wakuu wa nchi 10 za Jumuiya ya  Madola kilichomalizika jana.
Rais Kikwete alipokelewa uwanjani hapo na viongozi mbali mbali  wakiongozwa na Makamu Rais Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia aliungana na Rais  katika kuwaaga wahanga hao huku Ukonga Air Wing jijini Dar es salaam Miongoni  mwa waliohudhuria kuaga miili hiyo ni pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis  Mwamnyange,Inspekta Jenerali wa polisi Said Mwema na maafisa mbali mbali wa  jeshi.Miili hiyo ilitarajiwa kusafirishwa kwenda Mwanza,Musoma na Iringa kwa  ajili ya mazishi.
 Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Dar Es Salaam
 Tanzania
 11 Juni 2008
 The celebration of the ethiopia Millennium at the ethiopia embassy in London
Photos: Ayoub Mzee
Albino's Plight in Tanzania
http://www.nytimes.com/2008/06/08/world/africa/08albino.html?bl&ex=1213070400&en=751c11f3322c497f&ei=5087%0A