Wednesday, 16 March 2016

SUBASH PATEL WA M.M.I STEEL AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MABATI YENYE THAMANI YA SH.MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati yenye thamni ya sh.milioni 200 Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, 
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.
Wanahabari na wadau wa maendeleo wakiwa kwenye hafla hiyo ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumuzia changamoto ya madarasa katika wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.
Mwanahabri Renatus Mutabuzi wa Kituo cha Televisheni cha ITV akiwa kazini kuchukua taarifa hiyo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.

Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.

"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.

Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.

Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,  Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.

Tuesday, 15 March 2016

DC MAKONDA, GSM FOUNDATION WAZINDUA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI HOSPITALI YA RUFAA YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), ambaye mchana huu Rais Dk.John Magufuli amemteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam leo, ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine wadharura. Kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya, Mwakilishi wa Kampuni ya GSM, Deogratias Ndejembi ambao watajenga jengo hilo na kushoto ni Mhandisi, Hersi Said kutoka GSM ambaye atasimamia ujenzi wa jengo hilo.
 Ukataji utepe ukiendelea.
 DC Makonda akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa ujenzi huo.
 DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM Foundation. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya.
 DC Makonda akizungumza na wanahabari kuhusu ujenzi huo.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya akizungumza na wanahabari.
 Wanahabari wakichukua taarifa za ujenzi huo.
 Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation, Deogratias Ndejembi akizungumza na wanahabari kuhusu ufadhili wao wa ujenzi wa jengo hilo.
 Msingi wa jengo hilo.
  Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation, Deogratias Ndejembi (katikati), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda na Mhandisi atakaye simamia ujenzi huo kutoka GSM, Hersi Said wakionesha picha ya jengo hilo litakavyoonekana  baada ya kukamilika.
Taswira ya jiwe la msingi baada ya kuzinduliwa.



DC Makonda akiwa na viongozi wa Kampuni ya GSM mbele ya msingi litakapo jengwa jengo hilo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua ujenzi wa jengo la upasuaji katika Hospitali ya Mwananyamala ambalo litakuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za upasuaji kwa wajawazito na wagonjwa wengine wadharura.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake utaanza rasmi kesho, litakuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya upasuaji, uangalizi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wadharura (ICU) na uangalizi baada ya upasuaji na vingine kwa ajili ya utawala na huduma nyinginezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Dar es Salaam leo mchana  DC Makonda alisema kuwa jengo hilo litakuwa mahususi kwa ajili ya kupunguza idadi ya wagonjwa ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji kwenda Hospitali yaTaifa ya Rufaa yaMuhimbili.

“Kupitia jengo hili wajawazito wote na wagonjwa wengine ambao wanahitaji upasuaji watapatiwa huduma hiyo hapa hapa Mwananyamala. 

Alisema jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa 350-360 hivyo kwa kiasi kikubwa tutakuwa tumepunguza msongamano Muhimbili. 

Pia utakuwa tumefanikiwa kuokoa maisha ya wajawazito ambayo yameku wa yakipotea kutokana na kuchelewa kupata tiba,” alisemaMakonda.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa yaKinondoni, Dk. Azizi Msuya alisema jengo hilo litasaidia  kuokoa maisha ya wajawazito na wagonjwa wengine ambao  wamekuwa wakifariki kutokana na kucheleweshewa kupata huduma hizo.

“Katika wajawazito 100,000 wanaojifungua, 447 wanapoteza maisha. Sasa kupitia uwepo wa huduma ya upasuaji katika hospitali hii ya Mwananyamala tutajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kuokoa maisha  ya wajawazito hao wanaofariki” alisemaDkAzizi.

Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Foundation ambao ndiyo wafadhili wa ujenzi wa jengo hilo, Deogratias Ndejembi  alisema kuwa kampuni  hiyo imeamua kufadhili ujenzi huo ili kuokoa maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya upasuaji na pia kutokana nakuguswa na juhudi za DC Makonda.

“Kama GSM tumeamua kugharamia ujenzi wa jengo hili la upasuaji ili kuokoa maisha ya wanawake, watoto  na jamii nyingine ambayo imekuwa ikipoteza maisha kwa kukosa upasuaji. Pia juhudi na uchapaji kazi wa DC Makonda. 

Amekuwaakifanyakazikwajuhudikubwa, hivyo tukaona ni vyema tuka muunga mkono” alisema Deogratias Ndejembi.