Thursday, 26 March 2015

  Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu ufadhili wa masomo nchini China kwa mwaka 2015. Kulia ni Ofisa Habari wa Maelezo, Fatma Salum.
 Mwanahabari Salome Kitomari kutoka gazeti la Nipashe, akiuliza maswali katika mkutano huo.
Hapa mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale
WIZARA ya Nishati na Madini imetangaza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China kwa kipindi cha mwaka 2015.

Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo Badra Masoud Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wanahabari.

Alisema nafasi hizo za masomo ni ngazi ya Shahada ya Juu ya Uzamili katika fani ya gesi katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi cha China ambapo muda wa kutuma maombi hayo umeongezewa hadi kufikia Machi 30 mwaka huu.

Alisema waombaji wa ufadhili huo wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Ardhi au Uhandisi kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali, na muombaji awe na miaka kati ya 35 na 40.

Katika hatua nyingine Masoud alisema mitambo ya kuchakata gesi imekamilika kwa asilimia 96.

Alisema kukamilika kwa mitambo hiyo inamanufaa makubwa ikiwemo umeme wa uhakika na gharama nafuu kwani utekelezaji wa mradi huo utaliwezesha taifa kuokoa trilioni 1.6 kwa mwaka zinazotumika kununua mafuta kwa ajili yua kuzalisha umeme.

Masoud  alisema kukamilika kwa mradi huu kutachochea  maendeleo ya viwanda nchini kwani viwanda vingi vimeonyesha nia ya kutumia nishati  ya gesi asilimia  katika  kuendesha mitambo  yake  ya uzalishaji.aidha umeme wa uhakika utapunguza gharama za uzalishaji na kufanya  bidhaa za tanzania kukuzika katika masoko mbalimbali duniani.

Alisema tatizo la ajira nalo litapungua kutokana na kukamilika kwa mradi huu ambao utapelekea ajira  mpya  nyingi  kupatikana na kutokana na kuwepo kwa umeme wa kutosha na uhakika katika viwanda ambapo  viwanda  vingi vitaanzishwa vilevile umeme utakwenda mashambani na kwenye biashara nyingine hivyo kwa namna moja ama nyingine ajira  zitaongezeka. 

Alisema gesi hiyo asilia pia hutumika kama malighafi katika viwanda mbalimbali kama,mbolea, kemikali,aluminiamu pamoja na kutengeneza vifaa vya plastiki uanzishaji wa viwanda vipya kutokana na matumizi ya gesi  asilimia kutachochea 

kukua kwa uchumi  wa nchi yetu na kwa upatikanaji wa ajira mpya nyingi kwa vijana wetu. 

Aliongeza kuwa Serikali kupitia wizara hiyo chini ya Mradi Endelevu wa Usimamizi wa Rasilimali Madini (SMMRP), inakaribisha maombi ya Ruzuku Awamu ya pili kwa wachimbaji wadogo nchini.

Wednesday, 25 March 2015

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko kutoka katika nyumba za watu katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji ya mafuriko wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Buguruni Mnyamani waloathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia wananchi hao.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na Wataalamu washauri mbalimbali wa Sekta ya barabara nchini (hawapo pichani) kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze utakaoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).

 Kiongozi wa jopo la Wataalamu washauri kutoka Korea, Kunho-Jung, akifafanua jinsi mradi huo utakavyoendeshwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi (PPP).

Wataalamu washauri kutoka Sekta ya barabara wakiwa katika mkutano kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar es salaam – Chalinze utakavyokuwa. Ujenzi wa barabara hiyo utahusisha barabara sita (6) kutoka Dar es salaam – Mlandizi na barabara nne (4) kutoka  Mlandizi- Chalinze.

Jopo la Wataalamu washauri kutoka Korea wakimsikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani) katika mkutano uliokutanisha wadau mbalimbali ya sekta ya barabara nchini kujadili upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara  ya Dar – Chalinze.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa kujadili kuhusu upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa ubia wa barabara ya Dar – Chalinze uliofanyika jijini Dar es salaam.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (mbele) akikagua mto Ng'ombe uliopo eneo la Mwananyamala Kisiwani, wakati wa ziara hiyo Nyuma yake ni Naibu Meya. Songoro Mnyonge.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimamba, Kata ya Makurumla, Mohamed shukuru akisisitiza jambo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuhusu mikakati wanayoifanya kuepuka mafuriko wakati wa ziara ya Meya huyo aliyoifanya katika Mtaa huo jana. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Diwani wa Kata hiyo, Rajab Hassan.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akimsikiliza Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati akimpa maelezo kuhusu mazingira ya Mto Kiboko uliopo katika Kata ya Tandale wakati wa ziara yake katika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Mkazi wa Mtaa wa Bahi, Jomo Macha akimueleza Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda athari za mafuriko katika Mtaa huo, Kata ya Makumbusho wakati wa ziara ya Meya huyo jana. Wengine ni Watendaji wa Manispaa hiyo na wakazi wa eneo hilo.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akitoa maelekezo kwa watendaji wa Manispaa hiyo kuhusu kutafuta ufumbuzi wa chemba ya majitaka iliyofurika katika Mtaa wa Balozi Msolomi wakati wa ziara yake. Kulia kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na watendaji wa Manispaa hiyo.

Monday, 23 March 2015

Mbunnge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimkaribisha mratibu wa msafara wa wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste kutomaeneo mbalimbali nchini, Mchungaji Bernedict Kamzee kutoka kanisa la Glory of Crist la mkoani Katavi. 



Akizungumza Mchungaji Benedickto Kamzee, kutoka Kanisa la Glory of Christ la Katavi, alisema wamefikia uamuzi huo wa kuja Dodoma kuonana na Edward Lowassa bila kushinikizwa wala kushawishiwa na mtu yeyote.

“Hakuna aliyetushawishi, hata siyo maaskofu wetu, hili suala halina msukumo wowote zaidi ya msukumo wa Mungu,” alisema Kamzee.

Kamzee alisema wachungaji hao wanatoka kwenye madhehebu ya EAGT, TAG, PEFA, KLPT kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akizungumza na ujumbe huo wa Wachungaji waliofika nyumbani kwake pamoja na mambo mkengine ni kumuombea baraka za Mungu katika safari yake ya matumaini.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Khamis Mgeja akizungumza jambo wakati kuwapokea wageni hao.
Wachungaji hao wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli mjini Dodoma.
 Maombi yalifanyika na Mchungaji Bernedict Kamzee aliwaongoza wachungaji wote katika maombi hayo.
 Maombi yakiendelea

Lowassa akiagana na wachungaji hao leo.


Sunday, 22 March 2015

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 
Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.

Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura. 
 KIONGOZI WA MACHINGA MKOA WA DODOMA ALISEMA HAYA